Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday 2 September 2010

UNAKUMBUKA YEKEYEKE?


Huu wimbo unaitwa yekeyeke aliyeimba anaitwa Mory Kante,ni moja ya nyimbo ambazo naweza sema hazipitwi na wakati kwangu.Mara ya kwanza kuusikia ilikuwa mwaka 1990 kwenye graduation ya mjomba angu huko unyalukoloni....watoto wote waliokuwepo hapo siku hiyo tukaambiwa tushindane kucheza YEKEYEKE atakae shinda atapata shilingi 5 si nikashinda bwanaaa... furaha niliyokuwa nayo hakuelezeka.
By then shilingi tano kwa mtoto ilikuwa kubwa sanaaa.
Kilichonifanya nikumbuke huu wimbo leo nikiwa kwenye bus pembeni yangu alikuwa amekaa kijana fulani hivi, nilishangaa huyo kijana aliponisalimia maana si kawaida ya wasweed kusalimia kama hamfahamiani...akasema yeye anatoka Australia: maongezi yalikuwa kama ifuatavyo, You are from Africa right? nikajibu Yap, Akasema i like African Music
Nikasema good to hear that,nikamuuliza do you know any artist? akasema I know Mory Kante...Nikaguna coz nilikuwa hata sikumbuki who is Mory Kante,akaniskilizisha ndio kukumbuka.I was like OMG!!! Umenikumbusha mbali sanaaaaaaaa.
Je wewe una wimbo wowote unaoupenda toka utotoni mpaka sasa?

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

mimi naukumbuka wimbo ambao mama yangu alikuwa anauimba kwa maana hiyo nilianza kuusikia tangu ninanyonya ziwa la mama, tangu nipo mgongoni, Simba wa nyika SINA MAKOSA WATAKAKUNIUA BURE MAMAAA......

chib said...

Yasinta, Mh!! Kesho utadai ulianza kusikia tangu ukiwa tumboni kwa mama yako, ha ha haa