Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 7 September 2010

WATU WENGINE WANACHEZEA UHAI!

Pombe sio chai jamani..., jamaa akiwa kapumzika baada ya kuelemewa na pombe.
Hapa akijitahidi kuinuka ili aendelee na safari yake, hivi inakuwaje mtu umelewa kiasi hicho alafu unathubutu kuendesha baiskeli? na usikute ni mume wa mtu na ana watoto, aibu gani hii?. Duuuh watu wanacheza na uhai.

6 comments:

Bennet said...

pombe sio chai, au jamaa alikwenda kwenye vibotoli maana kule ukali wa pombe unabadilika kila siku na kwa kila mpiko, hakuna standard ya mama muuza

Yasinta Ngonyani said...

Lakini pamoja na hivyo kesho tena atakwenda. Hapo ndo utapoamini mlevi ni mlevi. kaazi kwelikweli!!

SIMON KITURURU said...

Tukumbuke tu KATIKA MAISHA kuna sababu nyingi sana tofauti zifanyazo watu tofauti wanalewa na sababu zote si za kijinga.

Ukienda baa kama nimchunguzi utastukia kuna uwezekano ingawa wote uwaangaliao wanakunywa pombe ila sababu zilizo waleta baa unaweza kukuta ni tofauti na idadi ya utofauti wake inalingana na watu waliopo baa.


Mwisho, tafakari na BUSARA za wengi wakati wamelewa ni tofauti na kabla hawajalewa.

Huyo hapo Mzee pichani utakuta kesho yake anaweza asiwe anakumbuka kitendo hicho cha kuanguka na kama wamhusuo hawajakiona kitendo , hitimisho la tendo zima HILO linaweza likawa wala halitii aibu.

Si kuna uwezekano labda waliomlewesha ni mke wake na watoto kwa kuwa akilewa ndio huacha hela nyingi za matumizi nyumbani?


Ni moja tu ya Mtazamo!

emu-three said...

Unajua binadamu sisi ni viumbe wa ajabu, wewe unaona hiki kinanidhuru lakini unakitumia, mwisho wa siku ukianza kuumwa unalia na kusaga meno.

NAJUA WAJUA said...

eeh! kumbe ni mambo ya bwax hayo!!Hao ndio wanaoolewa na mateja.

chib said...

Tabu ya pombe za kampeni, zinatolewa bure, basi wale wajinga wanazifakamia mpaka na pombe zinawafakamia na wao. Sasa kwisha kazi