Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 28 October 2010

HALI ILIKUWA HIVII…..!!!

KABLA YA NDOA KATI YA PATRICK NA JONESIA WALIOKUWA WANAISHI MBEZI AFRIKANA:

Patrick: Dahh! Afadhali nilichoka kusubiri sana

Jonesia: unataka niende zangu jamani?

Patrick: hapana nani alikwambia?

Jonesia: Je wanipenda kwa dhati?

Patrick: Ndio, nilikuwa na nitaendelea.

Jonesia: Umewahi kutoka nje ya mapenzi yetu?

Patrick: La hasha siwezi na ni kwanini unajaribu kuniuliza swali hilo?

Jonesia: Unaweza ni busu?

Patrick: Kila nafasi utakayo nipa.

Jonesia: utanipiga

Patrick: hee hapana wacha uchizi dear!

Jonesia: Naweza kukuamini?

Patrick: Ndio mpenzi

Jonesia: Patrick mpenzi wangu.

BAADA YA KUFUNGA NDOA SOMA KUANZIA CHINI KURUDI JUU.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

uwiiii! hii kweli ni muhimu kuulizana kabla ya kufunga ndoa. Afadhali ulisema tusome kuanzia chini..lol

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

chib said...

Ha ha haa, nilihisi maneno yamebadilika nikirudi juu, lakini, la hasha. Kumbe maswali ni yaleyale, na majibu ni yaleyale ila majibu yanabadilika,
Weweeeeeeeeee