Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 4 October 2010

JAMANI HII NI ADHABU AU?

Watoto wa shule ya msingi wakiwa wamejitwisha mizigo ya kuni, wanakozipeleka mimi sijui....Sasa sijui ni adhabu au wanapeleka nyumbani na kama ni nyumbani wazazi wao wanafanya nini? Mimi nakumbuka nilivyokuwa darasa la tatu mpaka la tano nilikuwa nauza ubuyu wa mwalimu fulani hivi, na nikifanya kosa mwalimu huyohuyo alikuwa akinichapa na kunipa adhabu ya kumchotea maji ndoo tano nyumbani kwake. Nikikumbuka roho huwa inaniuma sana,huwa najiuliza kwanini nilikuwa nakubali kunyanyasika hivyo?
Anyway ilikuwa ni utoto na sikujua haki zangu kama mtoto.

3 comments:

Adela Dally Kavishe said...

huo ni unyanyasaji kipenzi inakera sana hapo unakuta hata chakula hajala.

Yasinta Ngonyani said...

Shule ya msingi! nakumbuka pia ukifanya kosa basi kama sio kusafisha viwanja basi kesho yake uje na mzigo wa kuni, matete au nyasi. Mweeh ! tumetoka mbali kaazi kwelikweli.

Chacha o'Wambura a.k.a Ng'wanambiti! said...

....hayo ni mapenzi kwa mwalimu na kwa wazazi...lol!