Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday 26 October 2010

JE NI MAPENZI AU UJAUZITO YAWEZA TUMIKA KUMTIA PINGU ZA MAISHA MWANAMUME……??



Ni kwanini tumekuwa tukiona akina dada wengi huwa na ujauzito wakati wakufunga ndoa?. Ambapo kidini ni makosa...
Hivi Ni ujauzito ndio huleta mapenzi au mapenzi huleta ujauzito ambapo jibu la hapo zao lake ndio huwa ndoa katika hali ya sasa.
Hapo zamani ilikuwa Mapenzi + Ndoa = Ujauzito lakini sasa mmmmmmmmmmh au ndio mambo ya shake before use?
Credit to MO blog.

3 comments:

emu-three said...

Kidini kwa kweli ilitakiwa ajifungue kwanza ndio ndoa iwepo, lakini siku hizi dini inawekwa kama fasheni tu!
Wengi wanakimbilia kuoana ili kukwepa kuambiwa umezaa bila mume, na hili linaletwa na huku kuitwako `kupimana kwanza' ...sijui!

Simon Kitururu said...

Mambo ya kucheki kama shemeji ni mtamu au vipi kabla ya kuingia kichwakichwa hayo!:-(

Lakini kumbuka sidhani kama Adamu na Eva walifunga ndoa kabla ya kuzalisha tunda na watoto wao labda walioana wao kwa wao na Mama watoto na Baba watoto wakikorofishana walikuwa wanakimbilia nyumba moja kwa kuwa BAU na BIBI waliluwa ni walewale.

Nachojaribukusema ni kuwa labda swala hili ni la kawaida - na wala sio la kushangaza kukuta Mme na Mke wanashindana vitambi siku ya ndoa.:-(

chib said...

Kitururu mh :-)