Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Friday 1 October 2010

MASWALI YA UCHAGUZI WA MWAKA HUU.

Wandugu nimetumiwa maswali yafuatayo na jamaa yangu mmoja ili nimsaidie lakini binafsi yamenishinda, nadhani atakuwa kapewa asignment katika hii kozi fupi ya maandalizi ya uchaguzi. Plz mchango wenu utanisaidia kumjibu.

1. Ni rais gani duniani anayeamini kwamba kukaa madarakani miaka mitano ni kujifunza ili baadaye ukipewa fursa ya miaka mingine tena aweze kuwa mfanisi?

2.Rais wa kwanza Duniani kuwa na rekodi ya kuanguka anguka mbele ya kadamnasi ni.....

3.Ni Rais gani duniani anaye amini kwamba suala la urais ni la kifamilia zaidi na siyo la kitaifa?

4.Rais wa kwanza duniani kutamka hadharani kwamba hajui umaskini wa watu
wake unatokana na nini, ni................


5. Rais wa kwanza anaechukulia wingi wa magari kama kipimo cha maisha
bora! ni.............

6. Rais wa kwanza duniani anaepata ulinzi wa nguvu za Giza.(mnajimu) ni..........

7. Rais wa kwanza Duniani aliyesema watoto wadogo wa shule kupata mimba ni
kiherehere chao ni...........

8. Rais wa kwanza anayeogopa kuwaburuza mahakamani mafisadi ila ana uwezo mkubwa wa kumuwekea fitina mwizi wa mke wa mtu ni.........

9.Rais wa kwanza duniani aliyetumia 60% ya mabango yote ya biashara nchini
kwake kujinadi wakati wa kampeni ni..........

10. Ni Rais gani Duniani ambaye kwa mtazamo wake anahisi kafanya kazi kubwa nchini kwake kiasi cha kujisikia fahari kubwa kumuandaa mwanaye ili naye siku moja afuate nyayo zake...............

11. Rais wa kwanza Africa kudanganywa vibaya mno na wasaidizi wake ni........

12. Rais wa kwanza kusini mwa jangwa la sahara kufanya safari nyingi za nje ya nchi ndani ya mwaka mmoja tangu aingie madarakaini ni..............

0 comments: