Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, 26 January 2011

MTANZANIA AFUNGWA MAISHA MAREKANI!!!!

Mfungwa wa kwanza katika jela ya Guantanamo kushtakiwa kwenye mahakama ya kiraia, Ahmed Ghailani kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani.

Hukumu hiyo ilitolewa na mahakama ya jimbo la Manhattan.

Ghailani alipatikana bila hatia mwaka jana, katika kesi ambayo alishtakiwa kwa mauaji pamoja na mashtaka mengine kuhusiana na mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 katika balozi za Marekani mjini Nairobi, Kenya na Dar es Salaam, Tanzania


Mchoro ukionyesha Mtanzania Ahmed Ghailani

Jopo la majaji hata hivyo limempata na hatia ya kufanya njama ya kuharibu majengo ya serikali.

Upande wa mashtaka ulijaribu kumshawishi jaji kwamba Ghailani alipaswa kuonewa huruma kwa sababu hakujua kuhusu njama hiyo.

Vile vile walisema kuwa Ghailani aliteswa na CIA baada ya kukamatwa.

Hata hivyo waendesha mashtaka walitaka apewe kifungo cha maisha gerezani huku wakisisitiza kuwa alijua kuhusu njama hiyo.

Akijiandaa kutoa hukumu yake, Lewis A. Kaplan alisema ilikuwa siku ya haki kwa jamii za watu 224 waliofariki kwenye mashambulizi ya bomu ya mwaka wa 1998 pamoja na wale wote waliojeruhiwa.

Kaplan alisema aliridhishwa na ushahidi aliopata kwamba Ghailani alijua kwamba watu wangekufa kutokana na vitendo vyake.

Ghailani alikamatwa nchini Pakistan mwaka 2004.

Alipelekwa kwenye kambi ya siri inayosimamiwa na shirika la Ujasusi la Marekani, CIA, kabla ya kupelekwa Guantanamo Bay, Cuba, mwaka 2006.

Baadaye alihamishwa hadi New York alikoshtakiwa.
Credit to BBC.

5 comments:

Swahili na Waswahili said...

mmmhhh sitoweza kuisahau siku hii nilikuwa nimejifungua mtoto wangu wa kwanza nipo nyumbni na mama yangu weee tulitafutana!!!!!!!!!!!!

EDNA said...

Swahili na Waswahili mimi niliona kama ndio mwisho wa dunia vile...

SIMON KITURURU said...

Mie nilikuwa Nairobi na nilipita mbele ya uliokuwa ubalozi wa Marekani kama nusu saa tu kabla hapajalipuka!

Ila kesi hizi mie zanitia wasiwasi kwa kuwa huwa napatahisia ni watokao nchi masikini ndio kirahisi wanapewa zaidi kibano na kutiwa hatiani!:-(

emu-three said...

Mimi hapo sijui, kwani nahisi watahukumiwa samaki wadogo huku makambale na mapapa yanapeta!

Najiuliza lile bomu la heroshima walihukumiwa akina nani!

Goodman Manyanya Phiri said...

Mwenyewe Bin Ladin ambaye inasemekana ni papa wa hii bahari ya mambo haya yuko huru kabisa na unaambiwa kweli-sikweli "familia yake tajiri na ile ya akinaBush ni rafiki wa kibiashara katika uuzaji wa silaha hizohizo zinajotumika vitani dhidhi ya magaidi wenye imani au siasa kali duniani".


WHO IS FOOLING WHO?

Mimi binafsi mtindo wa kushambulia Tanzania, Kenya na siku za majuzi tu, Uganda, unanichefua sana. Sijui nisemeje zaidi. Lakini watu wanaoshindwa kupata viongozi wa kweli mule nchini mwao, wasije wakaleta migogoro yao nakuja kupigana barani mwetu kutuumiza bure sisi bila hatia na wakome!


Siku hizi unaambiwa hata huko Palestina wale tuliokuwa tunafikiri ni viongozi wa wazalendo habari mpya zinafichuka sasa kwamba wenyewe ni vibaraka wa adui yao!

Hebu soma ukipata nafasi sehemu nyingi zenye kichwa cha habari "PALESTINE PAPERS".

Mfano:

http://www.sonomacountyfreepress.com/palestine/palesndx.html