WASICHANA wameendelea kuonesha makali yao katika masomo dhidi ya
wavulana baada ya kushika nafasi nane bora kati ya 10 kitaifa kwenye matokeo ya mtihani wa kidato cha nne........
Kutokana na matokeo hayo, wanafunzi wawili walioongoza kitaifa walielezea furaha yao wakisema siri ya mafanikio yao ni kujituma wenyewe, juhudi za walimu wao, mazingira mazuri ya shule pamoja na msukumo wa wazazi wao.
Wa Kwanza: "Siamini kabisaa, ila Mungu alikuwa akiniona nikisoma kwa bidii. Nimepata nguvu kubwa ya kuendelea kusoma kidato cha tano na sita na chuo kikuu.
Matarajio yangu ni kuwa daktari," alisema kwa furaha Lucy light.
Wa Pili: "Siri ni ufuatiliaji wa karibu wa walimu na Meneja wa shule.
Pia kujituma mimi mwenyewe, mazingira mazuri ya shule na uhamasishaji wa wazazi wangu, lakini pia siwezi nikasahau msaada wa sala," alisema Maria-Dorin.
Binafsi huwa nafurahi sana ninaposikia mtoto wa kike anafanya vizuri iwe shuleni,kazini au kwenye ngazi yoyote ya utawala....
WANAWAKE OYEEEEEEEEEEEEEE!
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
5 comments:
Wanawake oyee !
Kimaumbile ya ubongo wa binadamu, mtu wa kike anazo akili kuliko mtu wa kiume ikiwa tunazungumzia juu ya kuwaza au kupata suluhisho lolote lile.
Kwa hiyo binafsi sishangai kabisa wasichana wamepata kuliko wavulana na nawapa hongera sana! Nipe nafasi Dada mwenye-baraza hili nifafanue kidogo juu ya sayansi ya ubongo wetu kama wa kike au wa kiume.
Ubongo wa kushoto umetengwa kwa ubongo wa kulia isipokuwa pitia tundu fulani wataalam kuwita CORPUS CALLOSUM (na samahani kama SPELLING ni mbovu).
Sasa CORPUS CALLOSUM ya kike ni kubwa kuliko ya kiume na hiyo humsadia mtoto wa kike au mwanamama kupata suluhisho kwa urahisi kuliko mtu wa kiume kwani msichana/mwanamke anatumia kwa urahisi PANDE ZOTE MBILI ZA UBONGO kufikiria wakati sisi wanaume kidogo tunashindwa.
Chunga sana, lakini! Sisi "wavulana" tunanguvu zetu nasisi kiakili. Tunawashinda "wasichana" juu ya sehemu ya ubongo inaotumika kwa nidhamu na ndiyo maana tunaongoza duniani katika masomo yanaohitaji nidhamu kwa mfano: teknolojia yoyote ile, udaktari na sehemu nyingi zile ambazo zinahitaji somo la hesabu (MATHEMATICS).
Ubongo wa mwanamke ni kiboko kwelewa haraka na nahisi ndio maana "nyoka alimtanguliza Hawa kumweleza kuhusu yale matunda ya werevu" kwani nyoka alijuwa CORPUS CALLOSUM ya Adam ni ndogo mno kwelewa haraka!
MMMh, najaribu kujiuliza hawo wanafunzi wanatoka shule zipi? Maana kama alivyosema wa pili hapo, `mazingira mazuri' yamechangia kufaulu kwake, walimu wazuri nk...najiuliza hawa wenzetu wa kata, watafaulu lini na kufikia kiwangi hicho...kwanza anaamuaka asubuhi, hajui chai, anafika kituoni, anapambana na daladala, au kudandia malori kama wanaosomea shule za kata zilizojengwa kuelekea KISARAWE...anafika shuleni haoi, walimu hakuna, vitendea kazi hakuna...lugha nzuri hakuna...halafu unamlinganisha na hawa wanaosema `inatrenational school, au senta nani sijui...
Haya walionacho wataendelea kuwa nacho na kama huna ulie tu!
Kaka Goodman asante kwa darasa.
Emu 3...naungana na wewe naona hawa watakuwa watoto wa International school,lakini pia hata watoto wa shule za kata wanafanya vizuri licha ya kuwa wanasoma katika mazingira magumu.
Simon...umekubali wanawake tupo juu eeeh!
kuna kashfa moja kwenye hizi shule zinazoshindisha kuwa wanaiba mtihani na inadaiwa kuwa waedapo A' level huwa wanafeli vibaya hasa hawa wa st francis
Post a Comment