Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, 14 January 2011

MWAKA UMEANZA VIBAYA KWA WABRAZIL!


Zaidi ya watu 500 sasa wamekufa kufuatia mafuriko makubwa kusini-mashariki mwa Brazil, na kufanya tukio hilo kuwa janga la asili lililoleta madhara makubwa katika historia ya nchi hiyo.

Mvua kubwa zilizonyesha zimesababisha maporomoko ya matope kuelekea katika miji kadhaa, ambako maelfu ya watu wamekimbia makazi yao.

Polisi nchini humo imesema idadi ya watu waliokufa inaweza kuongezeka zaidi.

Waokoaji wamekuwa wakijitahidi kutafuta watu walionusurika katika maene ya vijiji vya mbali vinavyofikika kwa shida.

Idadi hiyo ya vifo sasa imezidi idadi ya vifo vilivyotokea kwa maporomoko ya matope huko Caraguatatuba mjini Sao Paulo mwaka 1957, ambapo watu 430 walifariki.

Wakati huo huo, nchini Australia katika mji wa tatu kwa ukubwa wa Brisbane, shughuli za kuusafisha mji huo kuondoa matope na vifusi zimeanza baada ya mafuriko kupungua.

Kwa kadri kina cha maji kinavyopungua wakazi wa mji huo wanaanza kuona hali halisi ya uharibifu, ambapo mali zaidi ya 30,000 zimeharibiwa.

Hata hivyo Idara ya Utabiri wa Hali ya Hewa imetahadharisha kuwa bado ipo hatari ya kutokea vimbunga.