Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Saturday, 29 January 2011

VUNJA MBAVU!


Jamani hii miito mingine kwenye simu inatuponza..!!! Jamaa mmoja alikuwa anapata kinywaji sehemu, akaenda msalani akaacha simu kwenye meza aliyokuwa amekaa.

Ghafla simu yake ikaanza kuita…..”NIBEEBE NIBEEBE NIBEMBELEZE UNIBEEBE… NICHUKUE UNIBEEBEE…” mtu mwingine akawa anapita kando ya meza hiyo akaisikia, akaibeba kweli….. nani wakulaumiwa…??? ha ha ha kibwagizo baada ya uchovu wakutwa nzima have a lovely weekend…..
Credit to Mohamed blog.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

we Edna wewe umenifurahisha kweli na jumamosi imekuwa murwa maana nilikuwa hoi hapa kazini.

chib said...

Wafikiri aliyebeba alikuwa anaufurahia wimbo... aaaa wapi, ni kibaka mzoefu tu.

Goodman Manyanya Phiri said...

Hapo basi nami kabisa umeniBEBAAA! Asante sana!


Lakini nikupe kiboko yake, Dada Edna na huwenda wewe na wasomaji wa blogu yako mtakuwa na wikendi njema zaidi.


Chunga sana! Ni burudhani safi sana ikiwa wewe kisu lakini ukiwa nyama unatamaani kumpiga mtu kofi baada ya hapo. Nayo inakwenda hivi:


Simu ya rafiki yako inalia na yeye papo hapo anakukabidhi na kukusihi:

"Huyu bwana anayepiga ni kero tu! Nisadie umwambie asipige tena kwani nimekwachia wewe simu; mimi mwenye-simu niko safarini kwenda Ulaya kurudi mwezi ujao."


NAWE KWA UUNGWANA UNARUKA TENA KIMCHAKAMCHAKA UMESHAJIANDAA KURUDIA ULE UONGO DHIDHI YA "JAMAA".

JAMAA swali lake lakwanza ni:
"Yuko wapi mwenye simu?"

WEWE unajibu:
"Amekwenda Ulaya ameniachia mimi simu yake."

JAMAA: "Amekwachia wewe kama nani? Wewe unajidai sana, siyo? Wewe unajifanya mwerevu nini?"

WEWE: "Hapana ...samahani sana... Mimi nikama ... mimi nikama mfanyakazi-mwenzie tu.."

PAPO HAPO UNAANZA KUPEWA VIDONGE KAMA HUJAWAHI KUTUKANWA. TENA JAMAA LINAKWAMBIA SASA LIKO NJIANI KUJA KUKUPIGA KWANI LINAJUWA KABISA ULIPO NA "KWA HERI"!


Wakati ulipojibishana na yule "JAMAA", huku uliyekuwa unamstiri na kumwepusha TAYARI KESHA KUSANYA WATU KADHAA NA WAKATI WOTE ULE WALIKUWA WANAKUFAIDI JINSI JASHO LILIVYOKUWA LINAKUTOKA.

Kwanini lakini? Niulize!


Uliyekuwa unazungumza "naye" kwenye simu HAIKUWA SIMU ILIYOINGIA WALA HAIKUWA MTU WAKWELI BALI NI sound recording TU!

SIMON KITURURU said...

:-)

Swahili na Waswahili said...

hahahahaha da Edna singeibeba tuu ikinyaza airudishe!