Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 1 February 2011

BAJAJI,

Wabongo kwa kutunga majina? nilishangaa nilipoambiwa aina hii ya viatu inaitwa bajaji, mmmmh mimi ninavyojua Bajaji ni aina ya usafiri ambao upo kama baiskeli au pikipiki,sasa sijui hivi viatu vinauhusiano gani. Alafu jamani hivi viatu sivinafanana na vile vya miaka ya nyuma ambavyo vilikuwa vikiitwa utanikoma saa nane? hahaaa i had these kind of shoes, jua lile la saa nane likikolea viatu vinakuwa vya motoo hapo sasa utatamani ardhi ipasuke.

Hii ndio bajaji yenywewe sasa.....sasa jamani kuna uhusiano wowote hapa?
Kama mdau unafahamu kuhusu hili tuambizane basi .


7 comments:

Swahili na Waswahili said...

KWIKWIKWIKWI!! labda huo uwazi dada Edna,je unaijuarobot wewe au pan`chun`chu?umenikumbusha mengi sana mwenyewe nimevaa sketi yangu ya bluu,shati jeupe sox nyeupe nimepandisha mpaka magotini,chini utanikoma saa 8 halafu begani nina mfuko wa kibaharia!!pasi nguo karibu ziungue wangu naenda zangu Msimbazi Mseto hahahahahhahha ohhhhhhhh!!!!
Asante da Edna!!!!!!!!

SIMON KITURURU said...

DUh! Nilikuwasijui jina hilo!:-)

Goodman Manyanya Phiri said...

Hapo nami umenikumbusha mbali.


Wacha nikupeleke hukohuko.


Pale Ubungo-Kisiwani ninaye mdogo wangu wakike, mtoto wa amu yangu; na mwaka juzi nilienda kuwasalimia.

Lucy alinivunja mbavu alipohadisia jinsi nilivyokuwa nampenda miaka ya 1987-1992 naye enzi hizo akiwa msichana kama umri miaka 5 hivi.

"Kaka ulikuwa unanibeba begani kabisa na unatembea nami hadi kituo cha daladala mpaka hapo uliponinunulia BAJAJI"

Nami nilikuwa nimeyasahau yote hayo. Lakini nilipomwuliza: "Je,BAJAJI ndio nini?" aliniambia ni aina fulani ya vyatu.

Naleo nimeviona kabisa Asante sana. Nimepakumbuka tena Bongo, maana yake "usiache BAJAJI kwa msala upitao" (LOL)

chib said...

Hilo jina ndio kwanza ninalisikia leo!

emu-three said...

Ndio bongo hiyo, kila siku maneno mapya...leo ndata, kesho dingi, kesho kutwa, anajua mungu!

Anonymous said...

bajaj haina mlango hivi via2 pia havina kamba, bajaj ni fasta hivi via2 pia unaweza kuvivaa fasta.

John Mwaipopo said...

waswahili kwa kubatizana majina ama kubatiza vitu vingine hatujambo.