Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 7 February 2011

HATARIIIIII!


Haaaa! najaribu kujiuliza maswali majibu sipati...hivi huyo anayekojoa alikuwa anafikiria nini? na huyo anayenawa hakuona kama maji anayonawa yamekojolewa? Alafu ni watu wazima wangekuwa watoto ningesema huenda hawajui walitendalo.... Maradhi mengine huwa tunajitakia sisi wenyewe tena kwa makusudi.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Unafikiri Edna si uwongo maradhi mengine ni ya kujitakia kabisa. Kaazi kwelikweli!

Swahili na Waswahili said...

kweli hata hapo anahijika polisi asimamie?kama huyo baba anashindwa kujikinga mwenyewe nani atamkinga je ataweza kukinga familiya yake na kuwafundisha usafiwa mazingira na afya kwa watoto au jamii?

mmmhh mwenye nacho hakithami!!!!!

SIMON KITURURU said...

DUH!

emu-three said...

Mtu unaogopa kufa huku unakula sumu...mwisho wa siku unamuomba mungu..jamani tufikirie sana!

Goodman Manyanya Phiri said...

Nawe Dada Edna unavituko jamaani!

Mpaka umekaa ndani ya meli au chombo chochote kile ila uwapige picha jamaa bila wao kutahamaki hata kidogo?

Nangoja kwa hamu na matarajio makubwa kuona POSTI yako ifwatao je umetuiibia nini tena pitia LENS ya CAMERA yako!

Lakini, daima kosa litakuwa lakwako tu! Kwani hujawahi kusikia "usiyekiona hakikutendeka; nakama kimetendeka lakini hukwandika, basi hakimo kabisa katika kumbukumbu"?

Wewe endelea tu na hizo picha zako za kuonyesha watu wanakojoa hovyo; na utapelekwa huko mahakamani ya wakojozi bure! (LOL!!!!)

Lakini tukiacha vichekesho, umeonyesha jambo muhimu sana hapo na asante sana.Siku utakapokuja kwetu Afrika Kusini, naomba upige picha akinababa hapa Afrika Kusini wanaopenda kukojoa barabarani kuu za nchi hii.


Hawana aibu hata kama gari lingine linakuja wanakojoa mbele yalo tu. Hawana hata wazo ndani ya gari mule labda mnawatoto wakike wapi!


Tena usifikiri ni Waswahili pekee yao kama zamani kwakuwa walikuwa wamekatazwa kutumia vyoo vingi nchini kutokana na APARTHEID. Wazungu nao siku hizi wamekwishaiga mtindo huo wakukojoa barabarani mbele za magari bila kujistiri.

Aibu sana na natamaani ningekuwa mwanamke mie kwani wao hawafanyi kabisa upumbavu huo wamadume ya nchi hii!

EDNA said...

Hahaaa kaka MANYANYA PHIRI umenichekesha sana..nanukuu

"Wewe endelea tu na hizo picha zako za kuonyesha watu wanakojoa hovyo; na utapelekwa huko mahakamani ya wakojozi bure!"

Yasinta, Swahili na Waswahili, Simon, Emu-3 asanteni kwa kupita mahali hapa...