Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 21 February 2011

UKISTAAJABU YA MUSA…………………………!!!

-AKAMATWA NA POLISI KENYA KWA KUMLAWITI BABA YAKE.

Polisi nchini Kenya imemkamata kijana mmoja anayetuhumiwa kumdhalilisha baba yake anayeumwa katika eneo la Taita-Taveta.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 27 anatuhumiwa kumlawiti baba yake anayelala tu kitandani kufuatia maradhi katika kijiji cha Wesu divisheni ya Wundayi kwa kipindi muda wa miaka tisa, tukio ambalo limekuwa likitokea bila kutaarifiwa.

Polisi na Maafisa Afya wamesema baba huyo mwenye umri wa miaka 61 amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kiharusi na mara kwa mara amekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya wilaya ya Wesu.

Mama wa mtuhumiwa huyo amesema amelazimika kukimbia nyumba yao kwa hofu ya kuuawa na mtuhumiwa huyo.

Mama huyo amesema mara nyingi amekuwa akikimbia nyumbani hapo kufuatia mtuhumiwa huyo kutishia kumuua yeye pamoja na ndugu zake iwapo wangethubutu kutoa taarifa wa vyombo husika.

Polisi walipata taarifa za kufanyika vitendo hivyo kutoka kwa baba huyo mwenyewe wakati walipokutana katika hospitali hiyo.
Chanzo Mo blog.