Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday 29 March 2011

BARACK OBAMA ATETEA UVAMIZI DHIDI YA LIBYA........





Rais Barack Obama wa Marekani ameielezea operesheni ya kijeshi ya Odyssey New Dawn inayoendelea nchini Libya kuwa ni sehemu ya harakati zinazoenda sanjari na matakwa ya kitaifa ya nchi yake. Rais obama amesisitiza kuwa endapo hatua za kijeshi zisingechukuliwa, ingekuwa ni doa kubwa katika dhamira ya ulimwengu.


Ameeleza kuwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO itaanza kutimiza rasmi majukumu yake nchini Libya hapo kesho Jumatano. Hata hivyo Rais Obama ameahidi kuwa operesheni hiyo itachukua muda mfupi zaidi na gharama zake zitakuwa chache ikilinganishwa na vita vya Iraq.


Kauli hizo zimetolewa muda mfupi kabla ya kikao cha kimataifa kitakacholijadili suala la Libya kuanza mjini London. Mkutano huo utawaleta pamoja wawakilishi wa mataifa 35


WAKATI HUOHUO


Waasi wanaendelea na mashambulio yao yanayoelekea eneo la magharibi la Sirte anakotokea Kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi.


KATIKA HATUA NYINGINE


Wanachama wa Global Pan African Movement leo wanafanya maandamano ya amani wakipinga vitendo vya mataifa ya magharibi dhidi ya mgogoro wa Libya.


Akizungumza na waandishi wa habari katibu Mkuu wa Global Pan African Movement Stephen Othieno amesema uvamizi dhidi ya Afrika lazima usitishwe na mataifa ya Afrika lazima yasimame kidete na kupinga hali hiyo. Ameongeza kuwa hawata kaa kimya huku ndugu zetu nchini Libya wakiuawa.


Amesema maandamano hayo yatakayofanyika Pan African Square yanalenga katika kuonyesha ulimwengu kuwa kinachofanywa na mataifa ya magharibi dhidi ya Afrika hakiwezi kukubalika.


Credit to mo blog.com

0 comments: