Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 10 March 2011

AOA MBWA KUONDOA LAANA…!!! DUUUH DUNIA INA MAMBO.


Mwanaume mmoja katika jimbo la kusini la Tamil Nadu nchini India amefunga ndoa na mbwa wa kike katika harusi ya kitamaduni kwa lengo la kuondoa nuksi na laana.

Mtu huyo Selvakumar ambaye ni mkulima alifikia hatua hiyo ili kufuta uwezekano way eye kupata laana au kutokewa na jambo baya baada ya kuwapiga mawe hadi kufa mbwa wawili miaka 15 iliyopita.

Amesema anaamini kitendo alichokifanya kilimsababishia laana na amekuwa akipata mateso tangu wakati huo, ikiwemo kupooza miguu na mikono, kutosikia katika sikio moja na kushindwa kuongea vizuri.

Baada ya madaktari kushindwa kumpa matibabu kwa matatizo yaliyokuwa na mkabili, Selvakumar likwenda kwa mtaalam wa kusoma nyota ambaye alimwambia anasumbuliwa na laana ya wale mbwa aliowaua.

Mtaalamu huyo alimueleza kuwa hataweza kuepukana na matatizo yanayomsumbua hadi atakapo muoa na kuishi na mbwa ndipo laana hiyo itampitia mbali.

Kufuatia maelekezo hayo familia yake ilimtafutia mbwa wa kike aitwaye Selvi ambaye aliogeshwa na kuvishwa nguo kwa ajili ya harusi hiyo.

4 comments:

SIMON KITURURU said...

Mmmmh!

Anonymous said...

Hawa wadosi ni katika watu wachafu na wapumbavu duniani wana imani za kishenzi na kijinga.

Yasinta Ngonyani said...

eeehhh! jamani haya makubwa sasa na huu ni mwisho wa dunia !!!

Mija Shija Sayi said...

Unaambiwa yote ni imani yako tu, ingawa mimi naona kama anajiletea laana.