Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 22 March 2011

PADRI WA KANISA KATOLIKI ASHAURI WATANZANIA KUJIULIZA MASWALI 4 KABLA YA KWENDA LOLIONDO…!!!


Kiongozi wa Kanisa Katoliki Tanzania Kadinali Pengo.

Kiongozi mmoja wa kanisa Katoliki Jimbo Kuu la Dar es Salaam alielezea msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu tiba ya Loliondo inayotolewa na Mchungaji Ambikile Mwaisapile kuwa kabla mtu yeyote hajapata tiba hiyo lazima ajiulize maswali manne kwanza kabla ya kuamua kuitumia.

Akihutubia katika Ibada ya Jumapili katika Kigango cha Mt. Yohane wa Msalaba Parokia ya Mbezi Luis, Paroko wa parokia hiyo Padri Pengo alisema, “Sina chuki wala tatizo lolote na tiba ya Loliondo, lakini kama unataka kwenda lazima ujiulize maswali manne yafuatayo.

“Kwanza, tiba inayotokana na miujiza ya Mungu lazima iwe endelevu isiwepo kwa kipindi kifupi tu,” alisema.

Swali la pili alilotaka watu wajiulize ni kuwa tiba inayokuja kama muujiza kutoka kwa Mungu huwa na masharti? Swali la tatu alilolitaja Paroko huyo ambaye ni Padre wa Shirika la Wakalmeli ni kuwa, Kama tiba hiyo inafanyakazi ndani ya Loliondo, kwanini isifanyekazi Dar es Salaam na kwingineko?

Na swali lake la mwisho alilotaka watu wajiulize kuhusu tiba hiyo ya magonjwa sugu ukiwemo UKIMWI ni je, Mungu aliwaumba wanadamu na kisha kuamua kuwaangamiza? Au wanadamu wanaangamia kutokana na vitendo vyao vya ujanja ujanja?

“Ukiisha jiuliza maswali hayo na kujiridhisha kwa majibu utakayopata unawea kufanya maamuzi ya kwenda Loliondo. Hivyo ukiliona basi limeegeshwa katika stendi ya Mbezi au mahali pengine na ukasikia wapigadebe wanaita Loliondo Loliondo Loliondo, basi panda ukapate kikombe cha Babu,” aliongeza kusema.

Katika siku za hivi karibuni Mchungaji Mwaisapile ameutikisa Ulimwengu baada ya kutangaza kuwa anatibu magonjwa sugu kwa kutoa dozi ya kikombe kimoja cha dawa ya kienyeji kwa gharama ya shilingi 500/ kwa Watanzania na Tsh 1,000/= kwa wageni.

Viongozi mbalimbali wa siasa na dini wakiwemo maaskofu wa madhehebu ya Kikristo wamekuwa wakitoa ushuhuda wa ukweli wa tiba hiyo na kuwashauri wananchi wenye magonjwa sugu kwenda kijijini Samonge mkoani Arusha kupata tiba.Hata hivyo kwa upande mwingine baadhi ya viongozi wa makanisa hayo akiwemo Askofu Zakaria Kakobe wa kanisa la FGBF na Mchungaji Christopher Mtikila wamekuwa wakiipinga vikali tiba hiyo.

1 comments:

Rachel Siwa said...

Hayo ndiyo maneno yake 4,ukiyashika/ukiyaacha uwamuzi ni wako!
Asante da Edna kwa ujumbe!.