Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 14 March 2011

TAARIFA KUHUSU USALAMA WA WATANZANIA WANAOISHI JAPANI…!!!

JUMUIYA YA WATANZANIA JAPANI

Kumekuwa na wasiwasi mkubwa kwa Watanzania walio na ndugu, jamaa na marafiki nchini Japani juu ya usalama wao unaotokana na kutokea kwa majanga makubwa ya tetemeko la ardhi na Tsunami.

Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani (Tanzanite Society) kwa kushirikiana na mtandao wa Watanzania wanaoishi nchini Japani (wanatija), pamoja na ofisi zetu za ubalozi hapa Japani tunapenda kuchukua fursa kuwataarifu kuwa mpaka sasa tumeweza kuthibitisha kuwa karibu watanzania wote wako salama. Taarifa hii inamaanisha kuwa hatujapata taarifa zozote za Watanzania walioathirika na janga hili mpaka sasa zaidi ya uharibifu wa mali kutokana na tetemeko na tsunami. Tumeweza kuthibitisha kuwa watanzania walioko Fukushima na Sendai (maeneo yaliothirika zaidi) wote wako salama.

Tutaendelea kutoa taarifa kwa kadri tutakapokuwa tunapata habari mpya.

Kwa wale ambao wangependa kupata taarifa za ndungu zao tafadhali wasiliana nasi kwa kutumia anuani:chairman@tanzanitesociety.jp.

Utakapotuandikia tafadhali tupe taarifa zifutazo kama unazifahamu: Jina kamili, mji anaoishi na namba yake ya simu au anunai yake. Unaweza pia kutupa namba yako ili tuweze kukutaarifu kwa haraka.

Ahsanteni.

Uongozi.

Jumuiya ya Watanzania Wanaoishi Nchini Japani.

1 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Twamshukuru Mungu kwa hili na ahsante kwa taarifa.