Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 26 April 2011

CHEKA KIDOGO!

Kuna Mmakonde mmoja baada ya mkewe kujifungua mtoto wake alimwita Yesu, siku walipompeleka hospitali mambo yalikuwa hivi:

Daktari: Mtoto anaitwa nani?
Mmakonde: Anaitwa Yesu.
Daktari:Yesu?

Mmakonde: Eeh, anaitwa Yesu.
Daktari: Kwa nini unamwita Yesu na si jina lingine.
Mmakonde: Mimi naitwa Joseph na mke wangu anaitwa Mariamu mtoto wetu ataitwa nani?

Mganga: Sijakuelewa una maanisha nini?
Mmakonde: Hujanielewa nini, kwani Mariamu na Joseph mtoto wao si anaitwa Yesu? Mbona hamkuwauliza, unaniuliza mimi?”
Majibu ya Mmakonde yalimuacha hoi Daktari.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ha haaaa mweh! nimecheka kiduchu sikumbiki leo nimecheka mara ya mwisho...

Goodman Manyanya Phiri said...

Watu wengi kweli, Mmakonde Mwenzangu, wanafikiri jina la "Yesu" ni marufuku hata ikiwa wazazi sio JOSEPHI na MARY.


Ukweli ni kwamba siku zile za kuzaliwa Kwake, "Yesu" lilikuwa mojawake katika majina maarufu eneo hilo.


Hata wakati PONTIUS PILATE alipotaka mmoja katika Yesu na lijambazi moja asemehewe (Kitabu cha Matayo 27:15), aligundua wote wawili walikuwa wanaitwa "Yesu". http://www.sermoncentral.com/sermons/jesus-christ-or-jesus-barabas-jeremy-james-sermon-on-easter-resurrection-74034.asp


Mpaka leo binafsi nashangaa kwanini Waafrika wa kusini mwa Afrika wanaopenda kuiga vya mbali nao walilikwepa jina la "Yesu"


VIVA MAKONDE!!!

SIMON KITURURU said...

:-)

@Goodman: Halafu umestukia Amerika ya Kusini hasa ya waongeao Kispanish jina hili lilivyo la kawaida?