Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Sunday 15 May 2011

KAMA UMECHOKA NA KAZI ONDOA STRESS!

Wapenda ligi watatu walibishana kuwa nani
amekubuhu kwa ubishi kati yao . Wakaamua kila mmoja ahadithie ubishi wa haja alomfanyia mkewe ili wapime nani kubobea zaidi kwenye hiyo fani.

Mbishi 1 akasema:

Mi siku moja nilivyokuwa nje ya nchi nilimpigia mke wangu simu usiku akafungua simu hakusema haloo...kudadadeki! na mimi nikakaa kimya sikuongea mpaka alfajiri wakati simu ilikuwa wazi.

Mbishi 2 akatia:


Mbona hiyo cha mtoto, mi siku moja nimerudi home nikagonga mlango mke wangu akaufungua lkn hakusema karibu mume wangu...aliniangalia tu...nikaona analeta madharau! sikuingia ndani nikasimama hapo hapo mlangoni mpaka asubuhi...huyoo nikatimua zangu job.

Mbishi 3 akaunganisha:

Hiyo nayo mbona cha mtoto tu, mi mke wangu tulipooana alikuwa anaona haya kunigusa...ananidengulia eti! na mimi sikumgusa na mpaka leo hatugusani.

Mbishi 1 na 2:

Aaaaaaaah faza! acha usanii, nyie si mna watoto wawili lkn?

Mbishi 3:

Na hao watoto sijamuuliza kawaokota wapi...

kwani mi nataka mchezo!??.

4 comments:

emu-three said...

Duuh, hii inanikumbusha kile kisa cha Majuha, watatu...mmmh,kinasemaje vile...oh, baadaye bosi huyoooo!

Yasinta Ngonyani said...

Kaaaazi kwelikweli...Watu bwana mama weee mbavu zangu jamani..

Rachel Siwa said...

hahahhahhaa huyu mbishi wa 3 kiboko!!!!

EDNA said...

Asanteni wote kwa kupita mahali hapa.