Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday 26 May 2011

TANZANIA KUSHIRIKIANA NA SWIDENI KUPITIA UTAMADUNI KWANJIA YA TEKNOLOJIA.


Ushirikiano kati ya Programu ya Kiswidishi ya Teknolojia ya Taarifa na Mawasiliano ICT inayo ratibiwa na Idara ya Komputa ya Chuo kikuu cha Stockholm Sweden SPIDER kwa kushirikiana na Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni umetajwa kusaidia ukusanyaji na utunzaji na matumizi ya urithi wa utamaduni wa Mtanzania.

sehemu ya ukumbi wa maonesho wa makumbusho na nyumba ya utamaduni
Makubaliano ya ushirikiano huo yamefikiwa kati ya uongozi wa Chuo Kikuu cha SPIDER uliowakilishwa na Mkurugenzi wa SPIDER, DK PAULA UIMON na Mkurugenzi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni DK PAUL MSEMWA leo hii jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya makubaliano hayo Mkurugenzi wa SPIEDER DK UIMON amesema amefurahishwa na jitihada za uongozi wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni chini ya Rais JAKAYA KIKWETE kwa kusimamia vyema mradi mkubwa wa shirika hilo na kwamba ushirikiano huu utawanufaisha wanachi wa Sweden na Tanzania.

Kwa upande wake Mkurugeni wa Makumbusho na Nyumba ya Utamaduni DK PAUL MSEMWA amesema ushirikiano huo umekuja wakati muafaka ambapo shirika limejipanga kutoa elimu zaidi elimu ya Afya, Utamaduni na Sayansi kwa jamii.

0 comments: