Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 26 May 2011

KAMA VILE WANASEMA.........


Mvulana:Unajua mimi nakupenda sana wewe?

Msichana:mmmh najua mpenzi....

Mvulana:Nimeshawambia wazazi wangu tukisha maliza tu shule nakuchukua jumla.

Msichana:Mmmmh kweli mpenzi? maana warembo wako wengi huwezi badilika kweli wewe?

Mvulana:Aaaah wapi! wewe ni wangu wa kufa na kuzikana.Na ole wake nione kidume chochote kinakunyemelea, kipondo nitakachompa atajuta kuzaliwa.


Mdau ukiwa shule ulishawahi mpenda msichana/mvulana na mkaahidiana kuoana baada ya masomo? na je hiyo ahadi yenu ilitimia?

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Yaani Edna umeifanya Alhamis yangu ianze na kicheko. Hizo ahadi mmmhh mweh!.....

Swahili na Waswahili said...

hahahhahaaa wewe Edna wewe umewaza sana!!!!!!Naona ndani ya sketi kuna ka jiinzii nyeh kama si kunjombe basi ni sehemu nyingine zenye baridi.

SIMON KITURURU said...

:-)

emu-three said...

Duh, kama ahadi ni deni, basi wengi wana madeni hayo...mmh, mimi nakumbuka sikumuahidi mtu kihivyo...lol

Goodman Manyanya Phiri said...

Dume haliendi mbali lile, litaanguka kwa vyovyote tu!!! Wanawake hatari sana lakini tizama jinsi linavyotongoza na huku kamba la kiatu tayari kukanyagwa na jike!!!