Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday 13 June 2011

DAMBISA MOYO.


Anaitwa DR BAMBISA MOYO ni mdada anayejiamini, msomi,na ni mwanauchumi wa kimataifa, pia alitajwa na TIME MAGAZINE kuwa ni miongoni mwa watu 100 duniani wenye ushawishi (influential people).

Alizaliwa lusaka Zambia mwaka 1969,elimu yake ya juu aliipata Oxford University (DPhil)
Harvard University (MPA)na American University (BS, MBA).

Na pia ni mwandishi wa vitabu kama Dead Aid:Why Aid is Not Working and How There is a Better Way For Africa ,How the West Was Lost na The Stark Choices that Lie Ahead, ambacho kimetoka mwaka 2011.

Ni mdada ambaye kwa upande wangu huwa namhusudu sana kusikiliza lecture zake na pia kusoma vitabu vyake.

Mara yangu ya kwanza kumfahamu ilikuwa kwenye blog ya kaka SIMON KITURURU ambapo niliona video yake akiongelea uchumi wa Africa.Alinigusa sana nikaamua kumfuatilia kiundani zaidi.Kwa kweli nimejifunza mengi kupitia huyu dada, asante sana Simon kwa kuongeza idadi ya watu ninao wahusudu.

Msikilize hapa kidogo.

3 comments:

Simon Kitururu said...

Mdada Mkali huyu! Ila kuna wakaka kadhaa niliowahi kuongea nao wakadai kuwa huyu anafaa kwa wanamume kumuadimaya tu kwa pembeni ila kama MKE wanahisi atakuwa bonge la matatizo nyumbani!:-(

EDNA said...

Kwa hilo sishangai wanaume waliowengi huwa wanapenda kuwa na wanawake ambao wanajua itakuwa rahisi kuwacontrol,wakishajua wewe ni kichwa (yaani wewe unajua mengi kuliko wao),basi watakachokifanya ni kukutumia tu kimapenzi kuolewa itakuwa ngumu kama ulivyosema.

Simon Kitururu said...

@Edina: Sijui kama hilo lina ukweli kwa kuwa kwangu hata nikikutananaye leo naweza nikamchumbia akikubali kauli zangu.:-(


Ila ni kweli kuna wadau wangu wanasema huyo ukimwambia abinuke katika HATA starehe za kiutu uzima anaweza akahoji katikati ya shughuli ni kwanini ni yeye ilibidi abinuke!KITU ambacho kinaweza kuwa ni maji ya baridi kwenye mtafuta joto la utu uzima:-(