Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, 15 July 2011

KWA NINI WATOTO WADOGO HUJIFUNZA LUGHA NGENI KWA HARAKA KULIKO WATU WAZIMA?

Well,nimekuwa nikijiuliza mara kwa mara inakuwaje watoto wadogo hasa hasa wa umri kuanzia miaka 3 mpaka 10 hivi inakuwa ni rahisi kwa wao kujifunza lugha mpya/ngeni namaanisha mbali na lugha mama.

Sikuwahi kulifikiria hili mpaka nilipohamia hapa Sweden na kuona jinsi lugha inavyotutoa jasho.Labda nitoe mfano mmoja nina rafiki yangu kutoka Liberia yeye alikuja hapa Sweden na mtoto wake wa miaka 7,wameshaishi hapa kwa muda wa kama miaka miwili na nusu sasa.

Mama hawezi kuongea sentesi moja kwa kiswidi akaeleweka pamoja na kuwa amesoma kiswidi kwa miaka 2,na pia sio kwamba ni mbumbu ana master degree in political science aliyoipata huko kwao.

Mtoto wake anaongea kama vile amezaliwa hapa na ana lafudhi ya kiswidi kabisa.Huu ni mfano tu, wapo wengi au tupo wengi ambao tunajifunza lugha ukubwani inakuwa matatizo.So kama kuna lingustic yeyote ambaye anaweza kutupa sababu za kitaalamu atusaidie.

0 comments: