Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Friday 16 December 2011

DHAMBI NYEPESI SEHEMU YA PILI....byThomas Jordan.

Alianza safari yake na kuelekea sehemu asiyoijua huku akijipa matumaini kuwa atafanikiwa.

Ni asubuhi imepita sasa ni mchana denis yupo msituni pori la kutisha huku zikisikika sauti za ndege, sasa denis amechoka sana anaamua mchana huo bora apumzike, kwakua alizoea kuishi polini hivyo hakuweza kushinda na njaa kwani alitafuta kila aina ya matunda na kukaa chini huku akila matunda yake.

Alikaa pale kwa muda sana ilikuwa bado jioni bado kapumzika hatimae akapitiwa na usingizi, hakuweza kujizuia na sasa ni saa nne usiku bado kalala, saa sita usiku denis anashtuka, aliposhtuka alikuta kundi la watu wakiwa pembeni yake,denis alisema
“mnataka nini ondokeni kwangu”
Kimya kilizidi bila kujibiwa

“kwani ninyi ni akina nani? Bado hakujibiwa
“sasa usiku huu mnataka nini? Lakini ilisikika sauti ikisema
“tunataka kichwa chako”

Denis kusikia vile alishtuka sana na hakuwa na kingine zaidi ya kuokoa maisha yake ilimbidi akimbie, alikimbizana na wale watu kwa umbali mrefu sana na hata alipokaribiwa denis bila kujijua alijikuta ndani ya shimo refu huku juu likiwa limefunikwa na majani mengi yale ya kutanda,lakini walisikika wakisema wale watu mnaona uzembe tulioufanya.

Huu ni ujinga huku wakilisogelea lile shimo, denis alihofu sana kwani alijua uhai wake utaishia palepale kwa kuwa shimo lilizungukwa na majani mengi na ilikuwa ni usiku ilikuwa sio rahisi kujuwa shimo lile kulikuwa namtu walijuwa wameshamkosa na wakaondoka zao; denis ndani ya shimoalimshukuru Mungu.

“Nashukuru, eee…! Mungu nimeamini Mungu hamtupi mja wake”. Alivuta pumzi na kuishusha kwa kutetemeka, hii ni hofu aliyokuwa nayo kwani hakuamini kama amenusurika …….alisema tena,
“Kweli Mungu ashukuriwe”.

Hakuwa na jinsi ilimbidi afanye mbinu za kutoka humo shimoni, japo alihangaika sana lakini alifanikiwa na hakuweza kuendelea na safari yake huku njiani akiimba nyimbo ambazo alizipenda sana mama yake, wimbo ulisema;
“Bembea eee, bembea mtoto,
Bembea eee, bembea mtoto,
Nyamaza mwanangu kulia, bembea eee
Wanikumbusha ukiwa, bembea eee
Eee bembea mtoto …….

Sasa ni sa nane usiku bado yupo katika safari yake akijua wenda atafanikiwa, moyoni alijisemea,
“Hivi ni kweli nitafanikiwa kweli”,
“Eeh! Mungu naomba niokoe katika msitu huu”.
Kunyanyua shingo yake kwa mbali anaona mwanga pia alijiuliza “Kile ni nini?” aliendelea kusema;
“Au ndio wale watu walionifukuza kule wapo pale?”
“Hapana kwa kuwa kunakaribia kupambazuka ngoja nione kuna nini”.

Hivyo alilala palepale na ilikuwa ni sehemu ya mlima, hivyo ule mwanga aliuona kwa chini huku yeye akiwa juu ya huo mlima. Alilala pale kwa muda na hatimaye kunapambazuka huku akisikia kelele za watu, na hizi ni kelele za watoto bila shaka wanancheza huku watu wengine wakiendelea na majukumu yao.

Denisi anageuza shingo yake na kuilekeza upande huo, bila shaka denisi anafurahi sana kukiona kijiji kikubwa tena chenye watu wengi, kwa mbali anamuona mzee mmoja akivuta tumbaku na hapo denisi anapata akili na kujisemea,
“Ahsante mungu kwa kunifikisha hapa, naamini patanifaa, aliendelea tena kusema,
“Naamini eeh Mungu, nioneshe ndugu yangu”.
**********************************
Je Denis katika kijiji hicho atfanikiwa kumuona nduguye? Ungana nami simulizi ijayo yenye misukosuko zaidi.

DENIS ANAINGIA KIJIJINI.

Denis anaingia katika kijiji huku akiwa ni mtu mwenye furaha sana, kwani kunako kundi la watu alidhani angeweza kumpata dada yake, taratibu anamkaribia Yule mzee aliyemuona akiwa kule mlimani, anamkaribia na kumsalimia;
“ Shikamoo Mzee”, Denis alisalimu
“Marhaba” na ghafla Yule mzee akamkimbia, lakini denis alijisemea
“Ah! Kwani vipi! mbona ananikimbia”

Punde wakaja watu ni wanaume watatu na wanawake wawili, wakiwa wamevalia ngozi haya ni mavazi waliyoyazoea, walifika na kuweza kumkaribia Denis
“Mh! Hapana shaka hawa ni maaskari” nilijisemea kimoyomoyo na waliniuliza….
“Wewe ni nani na unataka nini?”

“Mimi naitwa Denis na sipo hapa kwa ubaya” alijibu na kusema tena
“Nimetokea mbali sana na ninaomba hifadhi yenu”
“sisi hatuwezi kukupa hifadhi labda twende kwa malkia wetu”, walimchukua na kumpeleka hadi kwa malkia wao.

“Jambo mkuu ee Malkia wetu mtukufu” walisalimu huku wakiinama
“Jambo, kwani kuna nini asubuhi yote hii?”
“Malkia wetu kuna mtu nimekuletea huyu mgeni katika himaya yako” …..

“Na isitoshe anaweza akatudhuru kwani hatumjui”
“Je mnaweza kunimbia mmemtoa wapi mtu huyu?”
“Ndiyo mkuu, kwani tumemkuta tayari ameshaingia kwenye himaya yako”. Bila kuchelewa malikia aliamua mtu huyo apewe adhabu.

“Hebu mpelekeni katika lile shimo humo ndimo yatakuwa maisha yake”
“Oh! Naomba mnisamehee mimi si mtu mbaya” aliongea denis
“Hebu tii amri, haya haraka twende” waliweza kumpeleka kunako lile shimo na kumtumbukiza humo, tena shimo refu na lenye kujaa uchafu yaani kila aina ya takataka.

“Oh! Sijui kama ndoto yanguitatimia” alijisemea Denis
Alikaa humo kwa muda wa siku nne bila kula chochote, kiufupi walishamsahau, lakini kuna mtu anasogea katika shimo lile ameshika kibatari na mfuko, huu ni mfuko wa ngozi ya ngomb’e anfika katika shimo lile na denis aliweza kusikia vishindo vile na kuinua shingo yake juukuangalia ni nani?

“kaka najua unanjaa sana hebu chukua chakula hiki
Ahsante sana dada ,kwani wewe ni nani? Denis aliuliza
“mapema sana kunijua lakini usijali”
“nashukuru sana”
Nilikula chakula kile kwani nilikua nina njaa kali sana na sikuamini kama ningeweza kupata chakula kile hakika nilishiba sana mpaka hatua ya kupata usingizi na kuweza kulala.

Ni siku nyingine nikiwa na siku tano ndani ya lile shimo kwa mbali nasikia vishindo vya watu vikikalibia lile shimo, niliinuka haraka kuufuata ule mfuko uliokuwa na chakula na kuwezakuuficha ………….

“habari zenu.’’niliwajulia hali
“sisi hatujambo, hujambo wewe mfu hai” huku wakicheka.
“Unaitwa na malkia wetu”
“Sawatunaweza kwenda”niliwajibu
Walimtoa ndani ya shimo na kumpeleka kwa mkuu wao.
Wakiwa kwa malkia ……..

“Hebu niambie umetokea wapi na unataka nini? Malkia aliuliza
“ki ukweli sijui nitokako na walaniendako”
“we ni mtu gani unaeishi bila kujua eneo lako unaloishi’’?
“mimi nimezaliwa polini nimekulia, polini na simjui ndugu hata mmoja”
“kwani wazazi wako wapowapi?
“ni marehemu”

“ndiyo malikia’’
“Sasa umekuwa ukiishi vipi huko porini?........
“na hadi kufikia hapa umejuaje?
“nimekuwa nikishindia matunda, na safari yangu imeku….imek” alinyamaza ghafla
“Mbona huendelei kuongea?

“hapana kuna kitu nimekumbuka”
“kitu? Ni kitu gani”
“ni maisha tu”
“mpumbavu kabisa ndiyo kinachokufanya unyamaze”
“nisamehe mkuu.’’
‘’Inavyoonyesha wewe unakiburi sana, hebu mpelekeni mahala pake”malikia alisema.
“ndiyo mkuu” Askari waliitikia.

Bila kuchelewa walifanya kama walivyoagizwa na malkia wao na kumpeleka kunako shimoni,Huko denis hakuwa na jinsi ya kufanyahivyo muda wote alikuwa mnyonge, na mwenye mawazo mengi
“hivi ni maisha gani haya” denis alijisemea…….

“denis, denis,’’ sauti ilisikika ikiita niya yule dada
“ Naam, oh! Ni wewe”
“Habari yako denis”Nzuri tu sijui wewe ni nani?”
“Jamani umeshanisahau”
“mh! Hapana”
“ila”

“sijakusahau, kwani tumekutana tu hapo nje”
“Hujakosea ni mimi kwani na jana nilikuletea chakula siunakumbuka’’?
“ubalikiwe sana sikujuwa kama ni wewe kwani ni wachache sana wenye moyo kama wako”

“usijali denis tutazidi kushirikiana”
“Nashukuru ila naomba nikuulize swali”

“swali gani tena hilo denis”
“Ni dogo tu ila laweza kuwa la maana”
“Haya nakusikiliza uliza”
“Jinalako ni nani?

“oh! Jamani denis ni hilo tu!”
“Ndiyo ni hilo tu, kwani ni swali jepesi?”
“Mmh! Mimi naitwa……Oh Denis walinzi wanakuja tutaongea siku nyingine”.
Ilibidi Yule dada akimbie, huku nyuma Denis akibakijilaumu ni kwanini akumuuliza tokea mapema.

“Doh! Kweli mimi ni mzembe, swali kama lile ningemuuliza mapema”. Alijisemea.
Basi aliishia kujilaumu nahuku muda ukizidi kwenda, hadi kiza kinapoingia Denis alijionani mtu mwenye furaha kwani ilimzidi pale alipozidi kukumbuka yale mazungumzo aliyokuwa akiyaongea na Yule dada.

0 comments: