Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 12 December 2011

DHAMBI NYEPESI .


KATIKA ULIMWENGU HUU KILA MMOJA WETU AMEBARIKIWA KUWA NA VIPAJI VYA AINA TOFAUTI TOFAUTI,....ILA LICHA YA KUWA NA VIPAJI HIVYO SI WOTE WENYE UJASIRI WA KUSIMAMA NA KUONYESHA VIPAJI VYAO KWA JAMII INAYOWAZUNGUKA...SABABU HUWA NI NYINGI...

ANYWAYS, NIMETUMIWA HII HADITHI NA KIJANA MDOGO HUYO HAPO JUU (THOMAS JORDAN 0652396812),LENGO LIKIWA NI KUJIFUNZA KWA NJIA YA KUKOSELEWA PALE ATAKAPOKUWA AMEKOSEA KATIKA SAFARI YAKE YA UANDISHI.
NITAKUWA NAWARUSHIA KILA BAADA YA SIKU MOJA MPAKA ITAKAPOISHA...UNGANA NAYE ILI KUJUA ANAZUNGUMZIA NINI KATIKA HADITHI YAKE YA DHAMBI NYEPESI.
##### #####

Ni maisha ya kusikitisha sana hasa ukiangalia kwa maisha yetu ya kitanzania wengi wao tunakutana nao haya ni maisha ambayo alikutana nayo kijana mmoja anaeitwa denis na alijitoa mhanga kwa kila kitu kufanikisha maisha yake yanawekwa mahali pazuri.

Denis ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na moja na katika maisha yake yote hajawahi kugusa darasa hata moja lakini kwa misukosuko aliyokutana nayo na jinsi alivyoitatua ni kama mtu aliesoma kwani alijiamini kwa kila jambo
Je ni mikasa gani aliyokutana nayo?.......... fuatilia simulizi hii.

Saa kumi na mbili asubuhi jogoo anawika kuashilia kumekucha denis anaomba toka kitandani huku akijinyoosha viungo vyake vya mwili na kuelekea upande wa pili ambako dirisha lake lipo, analifungua na kumuona mama yake akifagia uwanja …………….,
“mama shikamoo”

“aah! Denis adabu gani,salamu dirishan?
Ilibidi atoke nje na kumkalibia mama yake.
“Shikamo mama”Denis alimsalimia tena mama yake
“marahaba, siku nyingine usirudie tena hiyo tabia”,
Sawa mama naomba nisamehe ,
Baada ya salamu Denis alimuuliza mama yake kuhusu ahadi ambayo aliahidiwa na mamayake ,

“mama leo ni siku ambayo uliniahidi naamini utanitimizia”
“kuhusu nini? Mbona sikumbuki?
“kuhusu historia ya maisha yangu”
“ohoo…! Hivi ilikuwa ni leo eeeee”
“Ndiyo mama, kweli wewe ni msahaulifu”
“Nilishasahau nisamehe mwanangu lakini ngoja nikueleze”
Mama huku akikumbuka machozi yakaanza kumtoka,
“Mama mbona unalia? Ukilia wewe mimi nitakua matatani”
“ni kweli denis lakini inasikitisha” Basi mama jikaze nyamaza kulia huku akimfuta machozi:”

“Denis mwanangu maisha yako yalikua na vikwazo vingi sana na haya ndiyo maisha yako tokea utotoni hadi hapo ulipo”: Akaanza kumsimulia
Mimi mama yako nimeishia darasa la sita (6) ni baada ya kupata ujauzito wako lakini kabla ya hapo nili……….nili……, Denis alidakia”ulifanya nini mama mbona unabahatisha?
“Wala usijali tuachane na hilo hebu tuendelee”

Ndipo nilipofukuzwa shule na kurudi nyumbani wakati huo tulikuwa tukiishi na babu yako yaani baba yangu mimi, nilikaa na mimba ile hadi muda wa kujifungua ulipofika na hata baba yako sikumtaja sababu mila na destuli za hapo kijijini zilikuwa haziluhusu kufanya mambo kama hayo tungali bado wadogo kwani ningemtaja tu! basi angeuwawa,”kabla hajamaliza Denis alimuuliza mama yake, “kwa hiyo mama! Baba yuko wapi maana nimekuwa nikikuona wewe tu:”
“Bado sijamaliza, mama alimjibu denis
"OK mama basi tuendelee”.

Hivyo nilijifungua salama palepale kijijini ,babu yako ndiyo mlezi na ulipofikia umri wa mwaka mmoja hali yako ilidhoofika sana kwani mzimu ulisha jua hivyo uliumwa sana na hata usiku hukulala ilikua saa saba usiku ulizidiwa sana paka tukakatatamaa tulidhani asubuhi hautaiona, tulihisi ungefaliki, ndipo juhudi za kumtafuta mchungaji aje kukuombea tulizianza na tukafanikiwa kumpata na alifika na kufanya hivyo nashukuru Mungu ulipata nafuu.

Lakini kazi ya kwenda kwenye mzimu ilibaki palepale kwani tulisha jua kuwa tumekiuka mila na desturi kijijini hapo ilitupasatuelekee huko na mizimu ilitupokea na kutusamehe hapo ndipo ilipokuwa salama yako hivyo uliwezakupona kabisa na tulirudi nyumbani salama muda ulizidi kwenda baadae ilipokuja kugundulika kwa baba yako ndipo viongozi walimfukuza na kumtupia porini.

Sikuweza kumuacha kabisa ndipo tulipotoroka nae na ndiyo maana mpaka leo tupo porini lakini haikuishia hapo baba yako alipooza ghafla na alishindwa kufanya kazi hivyo nilikuwa na majukumu ya kuwalea wote wawili .

Ukiwa na miaka miwili (2) baba yako alitutoka hukuwa na ufahamu hivyo nililazimika kuwalea mwenyewe na kaburi unaloliona hapo hilo ndilo kaburi la baba yako, niliamua kumzika hapa hapa nyumbani.

Namuda wote huo tulikuwa tunashindia matunda ya porini hadi nilipopata akili ya kujiimalisha zaidi kimaisha mimi mwenyewe kwani tulikuwa tukiishi kwa kuhamahama hadi nilipomzika hapa basi na kibanda cha kuishi nikaamua kukijenga hapa hapa:”, kwa kifupi ni hayo tu mengine nitakuelezea siku nyingine nikipata muda kwa leo tuishie hapa.”

Aliishia hapo kumsimulia na akamuahidi siku nyingine ataendelea.
“Ahsante sana mama japo hujanimalizia”
“usijali kwani nimesha kuahidi.”

Basi waliendelea na shughuli zao huku Denis akichanja kuni na mama akiandaa chakula cha mchana. Walikuwa na desturi ya kula mara mbili tu, hii ni kutokana na uhaba wa chakula zaidi, walikuwa wakishindia matunda.
“Denis mwanangu njoo tule”
“Sawa mama namalizia kuchanja kuni”
Alimaliza na kupata chakula. Muda ulipita jioni inaingia hatimaye giza nalo linaingia hii ikiashiria kuwa usiku nao unaingia hivyo walianza kujiandaa na kuweza kulala kwani walichoka sana.

Ni usiku, Denis katika njozi anaota,kuwa kuna mzimu unamtokea na unamwambia kuwa aondoke eneo hilo na aende kusikojulikana alistuka toka usingizini.

“Oh! Mungu wangu ndoto gani hizi”moyoni alijisemea lakini kwa mbali alisikia sauti ya mama yake ikimuita.
“De…de…..denis mwanangu” ikionesha kuwa amezidiwa”
“Naam …mama” bila kuchelewa aliingia chumbani kwa mama yake na kukuta mama yake amezidiwa sana,

“Vipi mama” kwa mshangao!
“Denis mwanangu hata sijisikii vizuri”
“Kwanini mama, mbona ghafla hivyo?”
“Naona maisha yangu yapo mikononi mwa Mwenyezi Mungu hivyo sina budi kukuaga”.

“Hapana mama usitamke maneno hayo, yananiumiza sana”.
“Naomba unisikilize mwanangu japo ni dhambi kumficha mtu ukweli, lakini naamini kwa Mungu hii ni dhambi nyepesi, kabla sijakuzaa wewe alitangulia dada yako, na hivyo hatukuwa naye kwani alipotea kwa mazingira ya kutatanisha na sielewi yuko wapi”

“Kwahiyo mama mbona hukunieleza toka mwanzo”?
“Naomba unisamehe mwanangu najua kuwa nilifanya makosa”
Denis aliuliza, “inamaana haieleweki aliko na walahakurudi tena”?
“Ndio, na ……nanao ..”

“Mama, …! Mama, ……! Tafadhali usiniache” alisikika akisema denis.
“ Hali ni mbaya mwanangu naomba umtafute dada yako”
“Sasa mamanitamtafutia wapi, sisi tuko porini hivi hakuna hata nyumba”
Mama alisema, “fungua hiyo kanga na uchukue hilo karatasi”.
Denis bila kuchelewa alifanya hivyo.
“Ndiyo mama, hii hapa ninayo”.

“Hiyo karatasi ifungue” Denis bila kuchelewa alifungua.
“Mwanangu najua huwezi kusoma, lakini yaliyoandikwa humo ni majina ya baba yako na dada yako” aliendelea kusema …….
“Baba yako alikuwa akiitwa Daniel Malingumu na dada yako ni Pendo”
“Sa…sas..sasa mama mbona sijajua bado” denis alisema.

Mama huku akizidi kutetemeka na kurusharusha miguu.
“si…sin…sina cha kusema naona malaika wanakuja”akizidi kusema
“Dee…denis”huku akikohoa denis mwanamgu naomba mtafute dada yako”
“sawa mama nitafanya hivyo:” lakini sijui nitampataje kwani….”kabla hajamalizia kusema.

Mama…..!mama…..!” Denis aliiita kwasauti ya unyonge na baadae akagundua kuwa mama yake hayupo duniani alikuwa ameshafariki alilia sana denis na kuona kuwa ni mpweke hivyo hana msaada mwingine tena.

Yapata saa tisa usiku huku kukikaribia kukucha alianza maandalizi ya mazishi ilimbidi achimbe kaburi la kumhifadhi mama yake usiku huohuo nakubaki amekaa chini karibu na makaburi hayo mawili ya wazazi wake huku akizidi kulia kwa uchungu.

Sasa kunakaribia kupambazuka huku denis akikumbuka ile ndoto yake iliyomuamulu aondoke eneo hilo.,
“Mungu wangu naamini wewe ndiyo mwokozi wa maisha yangu”,
Alisikika denis akisema huku akiendelea,……..
“Nakukabidhi maisha yangu,kwani ndiyo nayaanza”

“Amen”

0 comments: