Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Friday, 10 February 2012

MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2012 YALIKUWA NA VITUKO VYA AINA YAKE.

HUYU NDIYE ALIYONGEZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012 KWA MKOA WA DAR ES SALAAM..

Anaitwa Moses Swai kutoka shule ya Feza Boyz ambae alikua anachukua kombi ya Science...Moses ameeleza kua ndoto zake ni kuja kua Doctor japokua kwasasa anapendelea sana mambo ya I.T na kueleza kua amefurahi sana kwa matokeo hayo na kua ana plan za kuendelea na elimu yake ya A.Level.

WAKATI HUO HUO, kuna mwanafunzi mwingine yeye alipoona mtihani mgumu akaamua kuandika mistari ya BONGO FLEVA.Duuuh dogo ni nomaaaa.Soma alichokiandika hapo chini.

“nashukuru sana wote wanaosahihisha huu mtihani wangu, nitakapofeli nitaendelea na fani yangu ya bongo fleva, majita yangu yako levo za juu na sio East zuu, ukiona vyaelea ujue vimeundwa”

“acha utani my girl, unauja nyumbani umezizi, mwenzako huku naona sijiwezi, kazi hiyo ya kuzizi nakwambia ukweli mwanzo ulikua mzuri lakini mwisho ukawa mbaya”

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hakika nakupa HONGERA SANA MOSES NA NAKUONEA WIVU ILA ULE WIVU MZURI kazi nzuri sana umefanya.
Na nakuonea sana wewe uliyeandika bongo flava kwenye mtihani Duh!
Halafu Edna ni mtihani wa mwaka huu au mwaka jana nimeuliza tu kwa sauti.

EDNA said...

Ni mtihani ulofanywa mwaka 2011 matokeo yakatoka mwaka 2012.

ADAM MARINYA said...

Hongera sana mdogo wangu Moses kwa kuipa shule na familia yako heshima kubwa!!!!!big up janjaaaa