Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Thursday, 14 June 2012

NIMERUDI BAADA YA KUWA TANZANIA KWA SIKU KADHAA.

Nilifurahi sana kumuona mama yangu maana ilikuwa inanisumbua kuongea tu kwenye simu na kupata taarifa za maendeleo ya afya yake.Asante Mungu kwa  kuniwezesha kumuona kwa macho yangu. 
Kwa kweli acheni Mungu aitwe Mungu mama alikuwa hawezi kula mwenyewe kukukaa na hata kuongea,lakini sasa anaweza kukaa na hata kula mwenyewe.Nakuombea kwa Mungu akuponye ili uweze kutembea na kurudi kwenye shughuli zako.

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Nami naungana nawe kwa yote ulosema. Mungu twakushukuru kwa kila unalomfanyia mama yetu na tunaomba umponye kwa haraka... He we Edna usha rudi kumbe? jamani ...pia nashukuru kuwa ulisafiri salama na umerudi salama tutawasiliana.

Yasinta Ngonyani said...

Twamshukuru Mungu kwa yote na tuzidi kumwombea mama. Ahsante kwa kutushirikisha...Tutawasiliana ndugu wangu!!

Rachel siwa Isaac said...

Mungu yu mwema,Mwanakwetu, Tunashuru sana kama umerudi salama na mama anaendelea vyema,Pamoja sana katika Maombi na Mungu atazidi kumtendea, Pole sana mamii.

EDNA said...

Asanteni da Rachel na da Yasinta maombi yenu ndiyo yamefanya aendelee vizuri.

emu-three said...

Mnafanana kweli, mungu atamjalia afya njema.
KUmbe ulitua bongo, duuh,ningelijua mapema.

EDNA said...

Emu three ni lazima tufanane ni damu moja hiyo hahaaa...Yap nilitua bongo ila nilikaa wiki moja tu na wala hata sikuweza kutoka nje ya nyumbani mpaka naondoka,Mtu akiniuliza nini jipya bongo nitakuwa sina la kumjibu.

Sara Gau Goloka said...

Mungu mwema atazidi kupata afya njema