Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Sunday, 2 December 2012

Onyesho la Tano la Mwaka la Tanzania Red Ribbon Fashion Gala 2012 lakusanya Shilingi Milioni 72.

 Flaviana Matata.
 Mc’s wa Onyesho la Mavazi la Red Ribbon Fashion Gala 2012 Abby Plaatjes na Evance Bukuku wakikaribisha wageni na kutoa utaratibu wa shughuli nzima katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. Muasisi na Mwenyekiti wa Tanzania Mitindo House Bi. Khadija Mwanamboka (kulia) akimkabidhi cheti ushiriki kwa Meneja Masoko wa CFAO MOTORS Tharaia Ahmed (katikati).
 MC Evance Bukuku akinadi gauni lililovaliwa na Mwanamitindo Jennifer Bash lililobuniwa na Sherri Hill.
 Wanamitindo Flaviana Matata na Jennifer Bash wakipita jukwaani na magauni yaliyotengenezwa na mbunifu wa kimataifa Sherri Hill wakiyanadi kwa wageni kwa ajili ya kuchangisha fedha za kusaidia kituo cha watoto yatima cha TMH.
Wageni waalikwa waliotia fora katika maonyesho hayo ambao walinunua magauni ya Sherri Hill kwa shilingi Milioni 4.8 Anitha (Kushoto) na Milioni 4 Alma ( wa pili kushoto) ikiwa ni mchango wao katika onyesho la Tanzania Red Ribbon Fashion Gala 2012.

0 comments: