Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, 27 March 2013

HII NDIO TANZANIA YANGU ISIYOISHIWA NA VITUKO KILA KUKICHA

ABOMOLEWA NYUMBA NA KUCHOMWA KWA KUDHANIWA MSHIRIKINA ILEMI,MBEYA.

Wananchi wenye hasira kali wakianza kuvunja nyumba ya Bibi Huyo
anaedhaniwa ni mchawi...!


Mtoto wa Bibi Atukipile akiokoa vitu kadhaa vilivyosalia...!!


Bibi Atupele pembeni akiwa na Mjukuu wake kwenye picha
ya Pamoja...Bibi huyo anaedhaniwa Mchawi
Baada ya vitendo vya kichawi kukithiri kijijini hapo....
Ni Baada ya Mtoto wa Miaka 11 kupotea Ghafla baada tu
ya kuena kumsalimia Bibi huyo Nyumbani kwake Majira ya
Ya Saa 11 Jioni.....!!
Bibi Huyo mwenye Umri wa Miaka (60) aishie kata ya masewe
wilayani Ilemi Mkoani Mbeya...Jana alinusurika kifo Baada
ya wananchi wenye Hasira kali kuchoshwa na Vitendo vya
Kichawi vinavyoendelea kijijini hapo na vyoye Bibi huyo akiusishwa..

Walisema katika vikao kadhaa vilivyoitishwa mtaani hapo kwa
 ajili ya kutafuta mbinu za kupatikana kwa mtoto lakini Mwanamke
 huyo hakuonesha ushirikiano jambo ambalo lilizua hofu
 miongoni mwa wakazi hao hali iliyopelekea kuhisiwa 
kuhusika na tukio hilo.
  
Walisema katika kikao kilichofanyika Machi 23 Mwaka huu
 majira ya Asubuhi mtaani hapo wananchi hao waliendelea
 kusisitiza kuwa Mwanamke huyo achukuliwe hatua kwa
 kuwa ndiye anayehusika na upotevu wa motto ambapo
 iliamriwa kwenda nyumbani kwake kufanya upekuzi.
  
Walisema baada ya kufika nyumbani kwake na kufanya upekuzi
 walikuta vitu vinavyohisiwa kuwa vinahusika na ushirikina
 ambavyo ni vitovu vya watoto wachanga watatu ambapo 
Mwanamke huyo baada ya kuulizwa alishindwa kutolea 
ufafanuzi hali iliyosababisha wananchi kupandwa na hasira 
na kuanza kumpiga.
  
Kutokana na tukio hilo Kaimu Mwenyekiti wa Mtaa huo Nedy
 Mwamlima alimnusuru Mwanamke huyo katika kipigo
 kutoka kwa wananchi kwa kumpeleka katika kituo kikuu 
cha Polisi kwa usalama zaidi.  
Baada ya mtuhumiwa huyo kunusuriwa na kukimbizwa
 katika kituo cha Polisi wananchi hao hawakupoza jazba
 zao ambapo waliamua kuteketeza nyumba ya mtuhumiwa 
ikiwa ni pamoja na kufyeka mazao yaliyokuwa yamepandwa
 jirani na nyumba yake.
Hata hivyo hasira za wananchi hao hazikuishia hapo bali 
walimsakama Mwanamke mwingine aliyejulikana kwa jina la 
Agnes Sika ambaye ni mke wa Mchungaji wa kanisa la Pentecost
 Groly  kwa madai kuwa ni rafiki wa mtuhumiwa na amekuwa 
akimfichia siri.
  
Jeshi la Polisi liliwahi kufika eneo laTukio na kumnusuru 
Agnes asipatwe na madhara ikiwa ni pamoja na kutochomewa
 nyumba yake ambayo tayari wananchi hao walionekana 
kuikimbilia kwa ajili ya kutaka kuibomoa.
  
Aidha Jeshi la polisi linaendelea kumshikilia mtuhumiwa
 kwa ajili ya mahojiano zaidi pamoja na upelezi ambapo Baba
 mzazi wa Mtoto anayesadikiwa kupotea katika Mazingira ya
 kutatanisha akisema anamwachia Mungu  baada ya juhudi
 za kumtafuta kushindikana. 

3 comments:

emu-three said...

Swali ni je kama sio mchawi kweli itakuwaje, ukizingatia huo uzalilishwaji....Na huu uchawi kwanini usiboreshwe ukawa wa kisayansi, na uwe wa manufaa zaidi. Kwa mfano nasikia watu wanaweza kutembea na ungo, sasa kwanini wasiboreshe huo usafiri, tukawa tunasafiria kwa ungo. Tungewazidi hata wazungu...just imagine...mpo juu na ungo, ....Lkn kitu kikiitwa `uchawi' ..basi tena ni uharibifu tu.

Furaha Eliab said...

mpaka leo kunawatu wanaimani hizo by www.eliabu.blogspot.com

EDNA said...

Jirani Emu-Three hata mimi nimewaza hivyohivyo,ila itakuwa ngumu kwa serikali kuhalalisha kwa sababu wanasema uchawi ni kitu kisichonekana.

@Furaha Eliab-wapo sana hasa hasa vijijini.