Saturday, 26 December 2009
Raia wa Nigeria ajaribu kulipua ndege
Raia mmoja wa Nigeria anashukiwa kupanga njama ya kuilipua ndege iliyokuwa imewabeba abiria 278 na wahudumu 11 ikiwa inaelekea Marekani kutoka Uholanzi.
Mshukiwa huyo, Abdul Mudallab mwenye umri wa miaka 23 yuko chini ya ulinzi wa polisi.
Alisema alikuwa anapanga njama hiyo kwa niaba ya kundi la al-Qaeda.
Baadhi ya abiria hao walisimulia jinsi Abdul alivyoanza kujichoma mguu akinuia kulipua mabomu ambayo huenda yalikuwa yametegwa kwenye ndege ya Northwest Airlines nambari 253.
Kufuatia kisa hicho, Rais Barack Obama alitoa amri ulinzi zaidi uzingatiwe katika usafiri wa ndege.
Taarifa zinasema ndege hiyo ilikuwa imesalia na dakika 20 kabla ya katika uwanja wa Detroit hapo Ijumaa.
Abiria mmoja alisimulia jinsi alivyosikia mlipuko mdogo kisha akaona moshi na moto ukiwaka.
Wahudumu wa ndege hiyo walitumia chombo cha kuzima moto pamoja na maji kukatiza kile ambacho kingesababisha maafa makubwa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment