Sunday, 20 December 2009
UN yaafiki makubaliano ya Copenhagen .
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amefurahishwa na mpango wa Marekani wa hali ya hewa mjini Copenhagen na kuuita "mwanzo muhimu".
Alikuwa akizungumza baada ya wajumbe kupitisha muswada unaotambua makubaliano hayo, ambayo Marekani iliyafikia pamoja na mataifa muhimu ikiwemo China na Brazil.
Lakini Bw Ban amesema makubaliano hayo ni lazima yafanywe kuwa sheria itakapofika mwaka ujao.
Mapema mkutano huo ulionekana kusambaratika baada ya baadhi ya mataifa masikini kuukataa mpango wa kupambana na mabadiliko ya hali ya hali ya hewa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment