Wednesday, 6 January 2010
PIGGE AMERUDI TENA KUJIVINJARI PALE PALE ALIPONUSURIKA KUFA
Pigge Werkelin,akiwa na mke wake Monica na watoto Nicole 17,Wilda 2 na wa mwisho miezi 5.
Ikiwa ni miaka 5 toka maafa ya Tsunami kutokea ambapo maelfu ya watu walipoteza maisha miongoni mwao wakiwa ni Waswidish 500 walipoteza maisha nchini Thailand,huyo jamaa hapo juu yeye alinusurika kufa lakini alipoteza Mke na watoto wawili wa kiume.Baada ya kunusurika kufa akaona yaliyopita sindwele akaamua kuoa tena na kubahatika kupata watoto wawili tena hao wadogo,huyo binti mkubwa ni wa mwanamke.Licha ya kunusurika kufa huyu jamaa amerudi tena kujivinjari na familia yake mpya kwenye ile ile beach ambayo aliyopoteza wapendwa wake na yeye kunusurika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Wanasaikolojia wengi wanaamini kwamba wakati mwingine kurudi katika mandhari ambapo tukio la kutisha lilitokea kunasaidia kuponyesha majeraha ya kisaikolojia na kuleta ile inaitwa "closure". Wengi hurudi katika maeneo ya ajali mbaya za ndege, magari, meli, treni n.k. ili kupata ile hisia upya nao huondoka sehemu hizo wakiwa na nguvu mpya ya utashi huku wakiamini kwamba kuna sababu njema ambayo iliwafanya wao wapone na wengine waangamie.
il inahitaji roho ngumu kidogo.
Post a Comment