Ni kweli kwamba kuna uhusiano wowote kati ya tabia ya mtu na kabila lake? hususani kwa watanzania..Utakuta mtu akifanya jambo lisilo jema watu watauliza kwani ni kabila gani?
kwa mfano ukisema mwanaume fulani anapenda kupiga mke wake watu watauliza kwani ni mkurya?...Mhaya watasema Mhuni, watu wakutoka Sumbawanga na Tanga watasema ni washirikina, wachaga wanapenda pesa,wahehe wanapenda kujinyonga,Wasukuma ni wakarimu...
Swali ni wangapi tunasikia wakipiga wake zao na si wakurya? au wangapi wanatabia za kihuni na sio wahaya? na nani asiyependa pesa ukamsingizia mchaga ndie nayependa pesa pekeyake? na mengine meeeengi.
Nilipitia Blog fulani nikaona kabila fulani limeshambuliwa sana kwa tabia zao, nikawa najaribu kulinganisha tabia za watu ninaowafahamu na makabila yao nikaona ni tofauti na vile jamii inavyowachukulia.
Binafsi naamini tabia ya mtu haina uhusiano na kabila lake na kama kuna uhusiano basi ni kwa asilimia chache sana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
7 comments:
Edna hizo zote ni imani tu na pia bado tuna amini kuwa kupiga mke ndiyo uanauma na mke anaamini akipigwa ni haki yake.
Da Edna, hizo ni stereotypes tu na socially-constructed beliefs ambazo hazina kichwa wala miguu.
Sasa mwanamke akitaja tu kuwa yeye mkurya ama atoka Mara basi kama UCHUMBA ndo umekwisha kabsaa kwa kuwa ati Mara WAUAJI :-(
Tabia ya mtu ni hulka ya mtu kibinafsi zaidi na wala haihusiani na kabila.
Kwani ukeketetaji uko Mara tu? Mbona wachaga, wamasai na watu wa singida wanakeketana?
@Yasinta: Kuna baadhi ya wanawake wanaamini wa makabila fulani kuwa kupigwa ni kupendwa na wasipopata kipigo toka kwa wapenzi/waume wao huzusha kasheshe.
"yaani niishi na mume mwaka mzima hajanipiga, kha! Si ni sawa na kuolewa na mwanamke mwenzangu?" ni mojawapo ya madai....lol
Upo hapo?
Ni sawa na ukikutana na kila msomali basi umuite pirate, si unataka vita.
Watakaosoma ujumbe wako wa leo watakuwa wamekuelewa.
Kaka Chacha nakubaliana na wewe, ni Stereotypes. Au kuna hata kamsemo ka kiswahili kanasema Samaki mmja akiooza wote wameoza,mimi sikubaliani kabisa na msemo huu.Tabia ya mtu ni hulka ya mtu binafsi na sikutokana na kabila lake.
Da Yasinta kweli ni imani na ujinga eti Mume mpaka akupige ndio uamini kama anakupenda lol...
Chib tena umetoa mpya, msomali umwambia pirate anakupa na ticket yako ya kifo hapo hapo.
Nanukuu..."Wasukuma ni wakarimu..."
Hakuna cha kuongeza...
Post a Comment