Wednesday, 5 May 2010
Klabu za kucheka kuanzishwa Zimbabwe,
Wanawake wawili wana mpango wa kuanzisha klabu za kucheka Zimbabwe, nchi inayokabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi duniani.
Shilpa Shah na Celina Stockill wanaamini watasaidia watu kukabiliana na majaribu ya maisha ya Zimbabwe.
Hivi karibuni waliandaa warsha katika tamasha la kimataifa la sanaa mjini Harare, huku wakiwapa mafunzo ya kushawishi watu kucheka.
Bi Shah ambaye ni mkufunzi wa kucheka amesema, "Ukicheka-unabadilika; na wewe ukibadilika- dunia nayo hubadilika."
"Kwahiyo ni amani duniani, vicheko kwa Zimbabwe, kwahiyo tufurahishane na kueneza furaha."
Katika warsha zao, Bi Shah na Bi Stockhill hushawishi watu kushikana mikono, kila mmoja akiweka sura yake imchekeshe mwenziwe, na kulala sakafuni na kupiga miguu yao hewani.
Pia huwaambia wabirue mifuko yao ya susruali ambayo haina kitu na kila mmoja aanze kumcheka mwenziwe kwasbabu hana fedha, na kunyoosheana kidole huku wakichekana.
Mtu mmoja katika warsha hiyo amesema, “ Tunahitaji kucheka zaidi, hasa katika hali hii tuliyonayo Zimbabwe- ukiwa masikini, ni muhimu ujifunze kucheka.Mmmmmh hii nayo kali.
HAHAHAHAA TAZAMA HII CLIP,ORIGINAL COMEDY NA MWISHO WA DUNIA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
2 comments:
Jamani heee, I will suggest they should think a productive activity for the time being regarding the economic crisis they have, hizo klabu za kucheka zingekuja baadaye
Chib: kucheka nako ni njia ya kumaliza economic crisis at least kwa wanaowachekesha ama kuwafanya wenzao wacheke kwa sababu kama uko stressed na hiyo economic crisis na unataka afueni itabidi wakuchomoe vijisenti kidogo ili ucheke kiaina....lol
Post a Comment