Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Saturday, 8 January 2011

RAIS BARACK OBAMA APONGEZA ONGEZO LA AJIRA MAREKANI!!!



Rais Barack Obama.
Ajira ni moja ya ahadi ambazo Rais Obama aliahidi wakati wa kampeni zake,na ahadi hiyo imeonekana kutimizwa kwa kiasi fulani.
Rais Barack Obama wa Marekani amepongeza mwelekeo wa kuongezeka kwa ajira nchini humo na kutoa wito kwa wafanya biashara kuongeza uwekezaji.

Wito huo ameutoa kufuatia kiwango cha wasio na ajira nchini Marekani kupungua kwa pointi 0.4 hadi kufikia asilimia 9.4 mwezi Disemba mwaka jana, ambacho ni kiwango kikubwa kupungua kwa mwezi mmoja tangu mwaka 1998.

Idara ya Ajira nchini humo imesema nafasi za ajira 103,000 zilitengenezwa mwezi uliopita, japo idara hiyo imesema kiwango hicho ni chini ya makadirio yao.

1 comments:

emu-three said...

Angalau kuna ongezeko, je kule kusipo na ajira tutasemaje!