Ni kweli kwamba kuna uhusiano wowote kati ya tabia ya mtu na kabila lake? hususani kwa watanzania..Utakuta mtu akifanya jambo lisilo jema watu watauliza kwani ni kabila gani?kwa mfano ukisema mwanaume fulani anapenda kupiga mke wake watu watauliza kwani ni mkurya?...Mhaya watasema Mhuni, watu wakutoka Sumbawanga na Tanga watasema ni washirikina, wachaga wanapenda pesa,wahehe wanapenda kujinyonga,Wasukuma ni wakarimu...
Swali ni wangapi tunasikia wakipiga wake zao na si wakurya? au wangapi wanatabia za kihuni na sio wahaya? na nani asiyependa pesa ukamsingizia mchaga ndie nayependa pesa pekeyake? na mengine meeeengi.
Nilipitia Blog fulani nikaona kabila fulani limeshambuliwa sana kwa tabia zao, nikawa najaribu kulinganisha tabia za watu ninaowafahamu na makabila yao nikaona ni tofauti na vile jamii inavyowachukulia.
Binafsi naamini tabia ya mtu haina uhusiano na kabila lake na kama kuna uhusiano basi ni kwa asilimia chache sana.


















