Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Tuesday, 10 August 2010

Simu yamchengua Msambaa!


Baada ya kutokea msiba huko Lushoto walimtuma ndugu yao mmoja kwenda kuwajulisha ndugu zake waliokuwa nje ya mkoa wa Tanga. Mtani wangu Msambaa aitwae Abdalahaman Shemaonge, alikwenda kwenye ofisi za shirika la simu hapo Lushoto. Baada ya kutoa namba aliandikiwa, aliunganishwa na mjomba wake Juma aliyekuwa akiishi Dar es Salaam.

Baada ya kuunganishwa mambo yalikuwa hivi:
Juma: Juma hapa, naongea na nani?”
Shemaonge: Shemaonge, ni Juma?”
Juma: Ndiyo, shikamoo mjomba.”
Shemaonge: Marahaba, yaani twasikilizana Lushoto na Dashalama?”

“Juma: Ndiyo mjomba, habari za huko?”
Shemaonge: Nakwambia siamini macho yangu, yaani twasikilizana, ama kweli huu ni waya kwa waya.”
Juma: Mjomba dunia ya teknolojia hii, unashangaa simu tu, mbona kuna mambo mengi ya kushangaza.”
Shemaonge: Haah,si hadithi hii? Sauti yako naisikia vizuri kabisa kama upo sikioni pangu, eeh kweli mzungu mwendawazimu.”

Shemahonge kwa kuishangaa simu alijikuta anamaliza dakika zote alizolipia bila kutoa taarifa ya msiba. Kweli ushamba mzigo.

1 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ha ha ha ha Ama kweli nimecheka kweli hizi simu hizi kaazi kwelikweli...