Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, 3 November 2010

UMISS!!!!


Wanawake tunakazi kwelikweli,ona kalivyojikondesha.... Masikini usikute kana kunywa chai na biskuti kila siku lol.....,Ukimuuliza kwa nini amejikondesha hivyo atasema anataka kuwa miss au anataka aonekane ni mrembo zaidi.Mmmmmh mimi naona amepitiliza mno.

5 comments:

Adela Dally Kavishe said...

mmmh kwa namna hii my dia huo sio umiss bali tatizo

chib said...

Huyo ni mgonjwa jamani.
Ana anorexia nervosa

EDNA said...

Adela kweli mwenzangu huyu atakuwa na matatizo.

DR.Chib hata mimi nafikiri utakuwa ni ugonjwa.

SIMON KITURURU said...

Pamoja kuwa inaweza kuwa ni ugonjwa, mara nyingi katika nchi za magharibi huanza kwa kutafuta kuonekana mzuri kwa kuwa kwa wamagharibi wengi wembamba na uzuri huendana. Nili wahi cheki docu moja mwaandishi wa habari aliye kuwa kanona tu aliingia experiment ili aandikie stori hili tatizo . Mwishoni ikageuka kuwa alidaka vyote Bulimia na Anorexia mpaka ikabidi awe anatibiwa kikweli kwa kuwa alikuwa anashindwa kurudia tabia yake ya zamani ya kujiona mzuri wakati mmnono na sangara wamo. Na akawa anashindwa kwa hiari yake kujizuia kujitapisha baada ya kula kitu(Bulimia) na vitu kama hivyo.

Kwa hiyo haya mambo yapo na yanaweza kuanza kama utani. Na haki ya nani unaweza kujinenepesha ukaota bonge la kitambi halafu ukashindwa kukiua kirahisi kisa unashindwa kubadilika na kurudia staili yako ya maisha ya kabla ya kitambi.:-(

Upepo Mwanana said...

Nyie na hayo maneno sijui bulimia, anorexia etc......
Huyo dada anatisha jamani