Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 20 December 2010

KUMEKUCHA!


Ni saa moja na nusu asubuhi,Pilikapilika za kutafuta ridhiki zimeshaanza katika jiji la Dar es salaam....Haijalishi ridhiki yako unaipataje? cha muhimu ni kwamba mwisho wa siku kila mtu ameweza kupeleka mkono kinywani....Siku moja nilipokuwa nyumbani Dar es salaam asubuhi saa moja na nusu na mimi nikiwa kwenye mizunguko yangu nilikuta na na hii familia ikiwa imesimama katikati ya barabara, nilikuwa na shauku ya kutaka kujua ni nini wanafanya? nikawasogelea na kujifanya kama nimepotea mahali ninapokwenda hivyo naomba kuelekezwa, wakanielekeza, baada ya kuelekezwa nikawauliza wanafanya nini katikati ya barabara? na hawaoni kama ni hatari? wakawa kimya kwa sekunde kadhaa ndipo binti mmoja akaropoka na kusema sisi ni OMBAOMBA.Nikawauliza kwa hiyo nyiyi ni familia moja? wakasema ndio.Mnasoma? mama yao akajibu watasomaje wakati hata mahali pa kulala hatuna? Nilitamani kujua mengi kuhusu hii familia lakini muda ukawa umenitupa mkono..Kiukweli inasikitisha kuona familia yenye mabinti wenye umri wa kwenda shule wapo mitaani wakiomba.

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Unajua kuna wkati mwingine sisi binadamu huwa tunalalamika kuwa tuna matatizo mengi sana lakini kumbe kuna waliokuwa na makubwa hata kupita yako. Mara nyingi nimekuwa nikifanya safari katika mashule na kuona jinsi watoto wanavyotupa chakula mpaka utatamani kulia. lakini pia kuna msemo unasema huwezi kuwafikiria wanaolala njaa kila wakati unapoacha kwenye sahani na pia wala wasio na pa kulala. Maana mwisho utajikuta unachanganyikiwa....

emu-three said...

Sasa hawo mabinti mwisho wa siku itakuwaje, mijamaa yenye tamaa itawahadaa...jamani hakuna njia ya kuwachukua watu kama hawa na kuanzisha ajira ya aina fulani.
Kuna kufaigia barabara, kuna kilimia bustani, kuna matangazo ya biashara nk, tunaweza tukaanzisha NGO, ya ajira za zarura tukasaidiana kwa hili. Mpaka litokee lakutokea ili watu wajulikane wamesaidia au sio

EDNA said...

Yasinta: Waswahili wanasema aliyeshiba hamjui mwenye njaa..
EMU THREE:Kilichoendelea mimi na wewe hatujui ila wazo lako ni zuri kuwasaidia hawa watu hatuitaji kuwa mamilionea,Watu kadhaa wakijikusanya nakukusanya nguvu pamoja inaweza kuwa msaada tosha kwa hawa watu,licha kuwa huwezi kuwasaidia wote.

chib said...

Mbona mimi nawaona wana afya nzuri, hata na mavazi. Hakika hawa ni wavivu wakubwa.

SIMON KITURURU said...

Inasikitisha!:-(