Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Wednesday, 22 December 2010

MISHEMISHE ZA CHRISMAS KATIKA JIJI LA DAR ES SALAAM.

Huu ni mtaa wa kongo (KARIAKOO) Mtaa ambao hauna jumapili ,jumamosi wala sikukuu, wakati wote umejaa watu., mtaa ambao umejaa matapeli,wezi ukizubaa unaibiwa hadi nauli ya daladala, pia ukinunua kitu kariakoo inabidi uhakikishe kabla hujafika nyumbani,vinginevyo unaweza kununua viatu ukifika nyumbani unakuta ni makaratasi.. Mimi nilishawahi kuingizwa mjini miaka kadhaa iliyopita, nilinunua viatu vyeusi kufika nyumbani kufungua viatu ni vyekundu tena vyote vya mguu wa kushoto,Vioja vya kila aina hutokea mahali hapa. Ukiwa ndio msimu wa sikukuu (X-MAS) Wakazi wa jiji la Dar es salaam wako bize kujipatia mahitaji yao kwa ajili ya maandalizi ya Christmas. KAMA NA WEWE ULISHAWAHI KUINGIZWA MJINI AU KIOJA CHA AINA YOYOTE KILIKUPATA AU ULIONA NINGEFURAHI KAMA UNGESHEA NASI.

3 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Hee! kaaazi kwelikweli! Ahsante Edna na kutuhabarisha habari hii:-)
God jul!!

SIMON KITURURU said...

Hapo kuna mambo! Nasikia pia kuna WAFANYA BIASHARA wenye maswala ya kichawichawi sana pia hapo !

emu-three said...

Huu ni mtaa ambao ninaweza kusema serikali imeshindwa kuuzibiti. Unakumbuka kuna kipindi waliwekwa hata maaskari kulipalinda ili watu kama hawo matepeli na wafanya biashara waslioingilia hapo waondoke, ilikuwa kama nguvu ya soda, na kila soda ikiisha povu wanarudi. Kila mmoja (wengi) wana historia ya kutapeliwa hapo...
Na sasa hivii sio mtaa wa kongo tu, sehemu nyingi za Kariakoo hata barabarani watu wa namna hiyo wanapanga vitu vyao,nguo vyakula nk, ukinunua umeliwa...na cha aabu askari wa jiji wapo wao wansubiri watu hawa wajazane wapange biashara zao mwisho wa siku ile pofu ya soda ikilipuka tena ndio utawaona wanavyowapiga watu hawo kuwanyang'anya vitu vyao nk!
Uchaguzi umeisha...sasa sijui tusikilize! ...bado kuna aibu aibu ya kuwavamia hawa watu, siunajua tean ndio waliotoa kura, sasa ...ok tusubirie