*NI KADRI MIAKA INAVYOSONGA MBELE
*NI KWA MUJIBU WA UTAFITI WA WATAALAM
*HALI HIYO INATISHIA USTAWI WA VIZAZI VIJAVYO.
Matokeo ya utafiti yaliyotolewa mwezi April mwaka huu yanaonyesha kuwa kwa zaidi ya miaka 40 iliyopita wanawake barani Afrika wamekuwa wakizidi kuwa wafupi.
Katika utafiti ulioitwa “Heights of Nations” uliofanywa na Profesa SV Subramanian wa Chuo cha Afya ya Jamii cha Harvard, imeonekana kuwa wanawake wanaozaliwa Afrika katika kipindi cha miongo miwili iliyopita ni wafupi wakilinganishwa na mama na bibi zao waliozaliwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia.
Mchumi John Komlos amesema kuzidi kupungua kwa urefu wa wanawake wa Afrika kunahatarisha ustawi wa kizaji kijacho.
Komlo ameongeza kuwa urefu wa mtu mzima ni kipimo cha ubora wa maisha, kiwango cha baiolojia ya maisha na muda wa kuishi, hivyo urefu unapodumaa kuongezeka au unapoanza kupungua miongoni mwa vizazi ni ishara kuwa mambo yanakwenda kombo.
Profesa Subramanian na timu yake walichunguza urefu kwa wanawake 364,538 wenye umri wa miaka 24 hadi 49 katika mataifa 54 yenye kipato cha chini na cha kati.
Kati ya nchi hizo 54, nchi 14 zilikuwa na wanawake wanaopungua urefu,nchi 21 hazikuwa na mabadiliko na nchi 19 zilikuwa na wanawake wanaoongezeka urefu.
Nchi zote 14 zilizokuwa na wanawake wanaopungua urefu ni za bara la Afrika.
Utafiti huo umeonyesha miongoni mwa nchi za Afrika ni Kenya Na Senegal tu ndizo zilizoonyesha wanawake kuongezeka urefu.
Kenya umekuwa nchi bora barani ya Afrika na imeshika namba 9 miongoni mwa nchi zote 54, ambapo imeonekana wanawake waliozaliwa Kenya miaka 1980’s ni warefu kwa takriba 1.95cm kuliko waliozaliwa miaka ya 1950’s.
Urefu kwa wanawake umedumaa katika nchi 15 za Afrika zikiwemo Uganda, Congo Brazzaville, Lesotho, Zimbabwe, Swaziland, Togo, Ethiopia, Zimbabwe, Cameroon, Burkina Faso, Guinea, Tanzania, Ghana, Gabon na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR).
Uganda imeshika nafasi ya 16 kwa kufanya vibaya katika urefu wa wanawake kati ya nchi zote 54 huku Tanzania ikiwa ya 26.
Urefu wa wanawake umekuwa ukipungua katika nchi za Rwanda, Zambia, Comoros, Madagascar, Jamhiri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), Msumbiji, Nigeria, Chad, Namibia, Benin, Liberia, Mali, Niger na Malawi huku umekuwa ukiongezeka katika nchi za Nepal, India na Bangladesh.
Rwanda imeonesha urefu kupungua kwa 4.2cm kati ya wanawake waliozaliwa miaka ya 1950’s na wale waliozaliwa katika miaka ya 1970-80s.
Mmmmh hii nayo imekaaje wadau.
Credit to mo blog.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
1 comments:
Mvutio wa neno la Kiingereza "petite" (yaani "dogodogo") umekwenda wapi huko Uzunguni?
Mimi nafikiri: kinyume na mawazo ya hao watafiti, wanawake wa Kiafrika watazidi kuvutia ulimwenguni kote nasi tutapata mashemeji na wapwa kibao kutoka Ulaya, Asia, Amerika...
... au nimeipoteza pointi, Jamaani?
Kwamfano, sikuona nchi ya Afrika Kusini katika orodha ya watajwa, lakini nchi Ufalme wa Swaziland nimeyiona. Sasa niwaambieni cha kuwashangaza: HAMNA WANAWAKE WANAOSIFIWA KUOLEWA NA WANAUME WA-AFRIKA KUSINI KULIKO WA HUKO SWAZILAND NA NAULIZWA KILA SIKU ETI NILIMPATAPATAJE MKE WANGU WAPILI KUTOKA HUKO MBABANE?...leo nahisi nimepata jawabu!
Post a Comment