Wednesday, 21 September 2011
NI MDOGO KIUMRI LAKINI MAMBO YAKE MAKUBWA.
Tanzania imejaaliwa kuwa na wanamziki wenye vipaji hapa naongelea BONGO FLAVA....Kila kukicha wanaibuka wapya.Lakini tatizo linakuja katika kudumu katika fani hii...wengi wao huwa wanapotoka wanatoka kwa speed KALI jambo linalokufanya wewe shabiki kuwa na matumaini kuwa atafikika mbali katika safari yake ya kimziki,lakini matekeo yake huwa wanavuma miezi miwili mitatu baada ya hapo hawasikiki tena.
Maswali ninyojiuliza je? huwa wanaridhika na kile walichokipata kwa kipindi kifupi? au wanakosa sapoti/wafadhili? au wanakuwa wamebahatisha na si wasanii wa ukweli? au mziki bongo haulipi? nawaza tuuuu.Na wewe pia unaweza kuchangia.
Msiklize kijana mdogo,ASLEY-AKIKUMBIA *NAKUSEMAEA* hapo juu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
3 comments:
Kweli ni mdogo lakini mkali...nadhani wanaanza tu bila kuwaza sana huko mbeleni itakuwaje? nami nimewaza tu hapa...
kwa mtoto anakipaji, asiache shule tuu maana hawakawii kulewa misifa na kuacha shule!,da' Edna hayo uliyoyasema ndiyo chanzo cha kudoda wangu.
Nafikiri maswala ya kuibuka na kupotea ni ya DUNIA nzima katika sanaa.
Muziki na sanaa kwa ujumla sio lelemama kwa kuwa washabiki wako wanataka uwe fresh kila siku kitu ambacho si rahisi.
Pili kwa Bongo wasanii wengi wa BONGO FLEVA bila kuwa na timu ya maprojuza nyuma yao hawawezi kwa kuwa wengi wajuacho nikushika kipaza sauti tu . Kwa hiyo wakikosa wakuwasapoti hata kwa biti za muziki inakuwa imetoka hiyo hasa ukizingatia kuwa bado hailipi kihivyo .
Ni mtazamo tu!
Post a Comment