Bye bye 2013
Selfie
Msosi wa mwisho kwa mwaka 2013.
Tuesday, 31 December 2013
Tuesday, 17 December 2013
Ana kwa Ana na Mhe. January Makamba
Mahojiano na Mhe January Makamba Pt I
Mahojiano na Mhe January Makamba Pt 2
CODES;TASWIRA MDAU GERALD NGOWI ALIPOKULA NONDOZZ TOKA CHUO KIKUU MZUMBE TAR 6/12/2013
![]() |
| furaha ya kutunukiwa shahada zao wadau hawa wote wamebobea katika maswala ya uhasibu na fedha |
![]() |
| Mdau gerald nowi akiwa na mdau ernest chimaguli baada ya kutunukiwa shahada zao toka chuo kikuu mzumbe mwishoni mwa wiki iliyopita |
![]() | ||
| Gerald ngowi,harmestone njiro na ernest chimaguli wakipozi baada ya kutunukiwa shahada zao toka chuo kikuu mzumbe wakibobea katika uhasibu na fedha |
PICHA ZOTE NA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG
Monday, 16 December 2013
Kipindi cha familia kutoka Jamii Productuion...Kwanini wanandoa hutembea nje ya ndoa zao?
Karibu katika kipindi hiki cha FAMILIA kutoka Jamii Production.
Katika kipindi cha wiki hii, mjadala ulikuwa KWANINI WANANDOA HUTEMBEA NJE YA NDOA?
Mbali na washiriki waliokuwa studio, pia tuliweza kusoma maoni toka kwa wasikilizaji wetu wanaoacha katika kurasa zetu za FACEBOOK
Karibu uungane nasi.
Mbali na washiriki waliokuwa studio, pia tuliweza kusoma maoni toka kwa wasikilizaji wetu wanaoacha katika kurasa zetu za FACEBOOK
Karibu uungane nasi.
Ukiwa na maoni, maswali ama ushauri usisite kuwasiliana nasi kupitia jamiiproduction@gmail.com
[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Papa Francis atwaa tuzo ya PERSON OF THE YEAR 2013
Jumatano wiki hii, jarida maarufu
na kongwe duniani la TIME, lilimtangaza kiongozi wa kanisa Katoliki duniani
Papa Francis, kuwa mtu aliyekuwa na ushawishi mkubwa kwa mwaka huu wa 2013.
Tuzo hiyo, ijulikanayo kama PERSON
OF THE YEAR, hutolewa kwa mtu ambaye ametawala vyombo vya habari kwa mwaka
husika, iwe ni kwa mambo mema ama mabaya.
Mwaka jana, Rais Barak Obama alishinda tuzo hiyo kwa kutetea kiti chake cha urais nchini Marekani.
Na katika fainali ya tuzo za mwaka
huu, walikuwemo pia Rais wa Syria Bashar al Assad ambaye amekuwa akituhumiwa
kutumia gesi ya sumu kuua raia wake, pia mwanasayansi aliyevujisha siri za
serikali ya Marekani Edward Snownden, Rais Obama na wengine sita.Hii ilikuwa ripoti ya Disemba 14, 2013
Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Friday, 6 December 2013
R.I.P NELSON MANDELA YOU WILL FOREVER BE MISSED AND NEVER BE FORGETTEN.

“No one is born hating another person because of the color of his skin, or his background, or his religion. People must learn to hate, and if they can learn to hate, they can be taught to love, for love comes more naturally to the human heart than its opposite.” NELSON MANDELA
Saturday, 30 November 2013
[AUDIO]: Kuzaga kwa silaha za moto na kuongezeka kwa mauaji Tanzania
Picha kwa hisani ya thehabari.com
Si jambo geni tena hivi sasa nchini Tanzania kusikia fulani kashambuliwa au kauawa kwa risasi.
Silaha za moto hapa nchini hasa zile zinazomilikiwa kiholela zimekuwa zikimilikiwa na kila anayetaka... kama vocha za simu.Hata mtu mwenye uwezo kidogo, na asiye na sababu ya kuwa na silaha anaweza kumiliki silaha nyumbani kwake .
Bastola kwa sasa zimekuwa kama bidhaa ya utashi na watu wanazimiliki kama wanavyomiliki simu za mkononi.
Ungana na Sophia Kessy (L) na Mubelwa Bandio (R) katika sehemu hii ya kwanza kuangalia tatizo hili linaloonekana kuzidi kuathiri na kutishia maisha ya waTanzania wengi.
[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Miaka 50 tangu kuuawa kwa Rais John F Kennedy

Ijumaa wiki hii, Marekani imeadhimisha nusu karne tangu kuuawa kwa Rais wa 35 wa taifa hilo, John F Kennedy aliyeuawa Novemba 22, 1963 alipokuwa akisafiri kwenye gari la wazi jijini Dallas
Rais John F Kennedy akiwa katika gari la wazi muda mchache kabla hajauawa kwa risasi. Pembeni yake ni mkewe na mbele yake ni aliyekuwa Gavana wa Texas John Bowden Connally, Jr.ambaye pia alijeruhiwa katika shambulio hilo
Kwa wiki nzima, kumekuwa na shughuli mbalimbali kukumbuka tukio hili lililoshitua wengi nchini humo. Mambo mengi yametendeka. Vitabu vipya vimeandikwa na watu wamezungumzia kuuawa kwa Rais huyo pamoja na ufuasi alioacha kwenye uongozi mpaka sasa. Na kama ilivyotegemewa, Kengele ziligongwa, maua yaliwekwa kwenye kaburi, bendera zilipepea nusu mlingoti na nyimbo mbalimbali ziliimbwaRais Barak Obama, aliadhimisha kumbukumbu hizo Jumatano wiki hii kwa kuweka shada la maua kwenye kaburi la Rais Kennedy na pia kutoa tuzo za heshima kwa watu mbalimbali akiwemo Rais mstaafu Bill Clinton, mwanahabari maarufu Oprah Winfrey na wengine 14.
Rais Barack Obama (wa pili kulia) akiwa na mkewe Michelle, Rais mstaafu Bill Clinton (wa tatu kulia) na mkewe Hillary Clinton wakitoa heshima mbele ya kaburi la JFK jumatano wiki hii.
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 23, 2013Monday, 25 November 2013
Congrats my lil brother on your graduation day.
We are all happy for you Jackson......and we wish you nothing but the best.
Smile brother.... you have all the reasons to smile.
Jackson ambaye ni mdogo wangu wa mwisho wiki iliyopata alipata shahada yake ya ( bachelor of information technology)
Smile brother.... you have all the reasons to smile.
Jackson ambaye ni mdogo wangu wa mwisho wiki iliyopata alipata shahada yake ya ( bachelor of information technology)
Wednesday, 20 November 2013
Ana kwa Ana na Astronaut Dr Donald Thomas
Karibu katika mahojiano kamili na Dr Donald Thomas.
Mhandisi na mwanaanga wa Marekani
Katika mahojiano haya, Dr Thomas anaeleza historia yake na namna ambavyo ALIHANGAIKA NA KUVUMILIA kabla hajapata nafasi ya kufanya kile alichokuwa akikipenda zaidi.
Ilimchukua miaka 9 tangu ajaribu kwa mara ya kwanza mpaka achaguliwe, na katika miaka hiyo, alituma maombi mara nne.
Ili kuongeza nafasi yake kufanikiwa akaamua kuchukua madarasa ya urubani, scuba diving, kufundisha, kuongeza elimu na mengine ili kufanikisha kile alichotaka kufanya japo hakukuwa na uhakika wa hilo.
Lakini aliamini katika atendalo.
Pia ameeleza maandalizi wanayofanya na mafunzo wanayopitia kuanzia wanapochaguliwa mpaka wanapoenda kwenye mission hizo, hisia na uoga wake siku ya kwanza alipanda space shuttle. Amezungumzia safari nzima na shughuli kuanzia wanavyoondoka mpaka wanavyofika angani pamoja na changamoto za kuishi kwenye orbit. Kuanzia kupika mpaka kutumia choo. Na pia, namna alivyopokea taarifa za kulipuka kwa space shuttle Columbia. Shuttle aliyoitumia mara tatu kati ya nne alizokwenda kwenye orbit.
Baada ya miaka 20 aliyofanya kazi kama mwanasayansi wa NASA, na safari nne kwenye Orbit, akastaafu na sasa ni Mkurugenzi wa Willard Hackerman Academy katika chuo kikuu cha Towson hapa Maryland ambapo anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho
Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com

Nilipata fursa ya kuhojiana naye mwaka 2011
Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com
Monday, 18 November 2013
Dr Donald Thomas alipohojiwa na Jamii Production
Katika kipengele hiki cha HUYU NA YULE, wiki hii utasikia mahojiano niliyowahi kufanya na Dr Donald Thomas. Mhandisi na mwanaanga wa Marekani.
Ilimchukua miaka 33 kutimiza ndoto zake za kuelekea kwenye Orbit. Na baada ya kwenda kwenye Orbit mara nne, akastaafu na sasa anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho
Nilipata fursa ya kuhojiana naye ambapo alieleza mengi mema
Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com
Ilimchukua miaka 33 kutimiza ndoto zake za kuelekea kwenye Orbit. Na baada ya kwenda kwenye Orbit mara nne, akastaafu na sasa anahimiza wanafunzi wa chekechea kujiunga na masomo ya Sayansi na Hesabu kwa manufaa ya kizazi kijacho

Nilipata fursa ya kuhojiana naye ambapo alieleza mengi mema
Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com
Saturday, 16 November 2013
HUYU NA YULE: Mjadala kuhusu MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE.
Katika kipengele cha HUYU NA YULE, wiki hii tuliungana na VIJANA WATATU
Liberatus Mwang'ombe, Peter Walden na Ally Badawy kujadili MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE.
Ali Badawi (kushoto), Peter Walden (kati(na Liberatus Mwang'ombe (kulia) wakiendelea na mjadala ndani ya studio za Jamii Production
Ulikuwa ni mjadala mrefu na huru ambao ulikuwa na mengi ya kufunzana
Karibu uungane nasi
Wakati tukimalizia mjadala kuhusu MAJUKUMU NA WAJIBU WA KIJANA KWA NCHI YAKE, Peter Walden alimuuliza Liberatus Mwang'ombe swali kuhusu kufunguliwa kwa matawi ya vyama vya siasa nje ya nchi.
Liberatus ni Katibu Mkuu wa Tawi la Chadema hapa Washington DC
Hapo pakawa na ka-mjadala kadoooogo ambako hata Ally Badawy na mwongozaji wa kipindi Mubelwa Bandio wakachangia.
Karibu usikilize

[AUDIO] DAKIKA 90 ZA DUNIA: Hatari ya bunduki za kuchapishwa nchini Marekani
Bunduki ya plastiki iliyotengenezwa kwa mashine ya 3D ikifyatua risasi wakaati wa majaribio
Photo credits: Screenshot from ATF Video
Kama tulivyoripoti katika ripoti hii ya Septemba 21, mauaji ya kutumia bunduki ni kati ya matatizo makubwa nchini Marekani.
Lakini pia, uwezo wa nchi hiyo katika teknolojia umesaidia kupunguza madhara ya vifo hivyo kwa kuwezesha kukamatwa kwa silaha kabla hazijafanya madhara.
Hii inajumuisha pia kutumia vifaa maalum vya kugundua vitu vya chuma ambavyo mtu anaweza kuwa ameficha. Hata hivyo, kukua huko kwa teknolijia pia kuna athari katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Wiki hii, kitengo kinachojishughulisha na udhibiti wa Pombe, Tumbaku, Bunduki na Milipuko nchini Marekani (ATF) kimetoa ripoti kuhusu athari ama madhara yanayoweza kusababishwa na bastola za plastiki zinazochapishwa katika umbo halisi (3D Guns)
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com
JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"
www.jamiiproduction.blogspot. com
http://www.youtube.com/user/ mutwiba/videos
https://soundcloud.com/jamii- production
Photo credits: Screenshot from ATF Video
Kama tulivyoripoti katika ripoti hii ya Septemba 21, mauaji ya kutumia bunduki ni kati ya matatizo makubwa nchini Marekani.
Lakini pia, uwezo wa nchi hiyo katika teknolojia umesaidia kupunguza madhara ya vifo hivyo kwa kuwezesha kukamatwa kwa silaha kabla hazijafanya madhara.
Hii inajumuisha pia kutumia vifaa maalum vya kugundua vitu vya chuma ambavyo mtu anaweza kuwa ameficha. Hata hivyo, kukua huko kwa teknolijia pia kuna athari katika mapambano dhidi ya uhalifu.
Wiki hii, kitengo kinachojishughulisha na udhibiti wa Pombe, Tumbaku, Bunduki na Milipuko nchini Marekani (ATF) kimetoa ripoti kuhusu athari ama madhara yanayoweza kusababishwa na bastola za plastiki zinazochapishwa katika umbo halisi (3D Guns)
Hii ni sehemu ya ripoti ya Jamii Production kwenye kipindi cha DAKIKA 90 ZA DUNIA kinachorushwa na kituo cha Radio cha Capital FM cha Dar Es Salaam Tanzania kila Jumamosi kuanzia saa moja na nusu asubuhi (7:30 AM).
Bahati Alex (L) Capital Radio Jijini Dar es Salaam na Mubelwa Bandio (R) wa Jamii Production Washington DC
Hii ilikuwa ripoti ya Novemba 16, 2013Kwa maoni, ushauri, nk usisite kutuandikia jamiiproduction@gmail.com
JAMII PRODUCTION*
"Usahihi wa fikra ndio fikra sahihi"
www.jamiiproduction.blogspot.
http://www.youtube.com/user/
https://soundcloud.com/jamii-
Monday, 23 September 2013
HATIMAYE MANGULI KATIKA WIZI WA MTANDAO WAKAMATWA KATIKA OFISI ZA TIGO BUGURUNI
mrembo huyu ni mmoja wa watuhumiwa wa kesi hii ya wizi wa mtandao baada ya kutumia kitambulisho chake na kutaka kuja kurudisha line ambaye sio yake kwa kuahidiwa kupewa pesa kidogo kama ujira wake na katika melezo yake akasema hawatambui wahusika wenzake kwani amekutana nao tu sinza na wakampa dili hilo na kuamua kuchukua bajaji ambao iliwaleta mpaka ofisi za tigo buguruni rozana
huyu ndio staring mwenyewe aliyechonga mchongo wote na kumshawishi huyu mwanamke kutumia jkitambuluisho chake kufanyia wizi huo wa kimtandaO

mrembo akijitetea kuwa hahusiki kabisa katika wizi huu na pia kujitetea kuwa kaacha mtoto mdogo nyumbani

hapa akitoa mae4leoz kuwa yeye si mwizi na hwafahamu kabisa wahusika wenzaqke na yeye ni mfanyabiashara wa vipodozi![]() |

hiki ndio kitambulisho alichoktaka kutumia huyu mwanamke kuswap line ambayo sio yake lakini aliweka jina la mhusika wa line na namba alizokuwa anapiga maranyingi lainmi sura yake bahati mbaya kwa umakini wa mfanyakaiz mmoja wa tigo kwa jina octavian rweyendera alifanikiwa kubaini udanganyifu huo na kuamuru awekwe chini ya ulinzi mara moja
aliyesimama hapo yeye alibiwa kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking ya NMB baada ya line kuharibika ghafla kumbe mmoja wa watuhumiwa alirenew na kuiba pesa 
hiki pia ni kitambulisho cha mteja huyo hapo juu aliyeibiwa pesa kwenye acount yake ya NMB kiasi cha milioni moja kwa njia ya sim banking baada ya mmoja wa hawa watuhumiwa kuja kurudisha yake hii kwa kutumia kitambulisho hiki ambacho kimetengenezwa kwani si halisi na hatimaye kufanikiwa kuiba pesa kwa sim banking baadae

hapa mtuhumiiwa mmoja akiwan kajilaza chini kwa kugoma kutoa maelezo kwa walinzi waliowaweka chini ya ulinzi

hapa huyu binti KILIA kwa uchungu na kuomba asamehewe

wakiwa ndani ya gari ya polisi kuelekea kituo cha polisi buguruni![]() |
umati wa watu uliofurika kushuhudia tukio hilo la aina yake ![]() |

Askari polisi wakisikiliza kwa makini jinsi watuhumiwa hao walivyokamatwA
PICHA NA HABARI NIMETUMIWA NA MWANAHARAKATI MZALENDO BLOG
Subscribe to:
Posts (Atom)