Tuesday, 29 May 2012
BRAND NEW VIDEO....SHETTA FT DIAMOND,NIDANGANYE
Nimependa maneno ya huu wimbo,kuna wakati unaweza ukaona ni kheri ukiambiwa uongo kuliko ukweli ilimradi tu usiiumize nafsi yako.Hili labda huwa linajitokeza sana ukiwa kwenye mahusiano ya kimapenzi,unaweza kusikia kuwa mpenzi wako ana mtu mwingine roho ikakuuma na kuamua kumuuliza mpenzi wako kwamba yanayosemwa ni kweli? Nadhani akijibu NDIO moja kwa moja utaumia zaidi kuliko akikudanganya na story za sungura na fisi.Ila binafsi ningependa kuambiwa ukweli sababu najua nitaumia kwa muda then maumivu yataisha na maisha yatasonga mbele.
JOYCE KIRIA- KUTOKA U'HOSEGIRL MPAKA UTANGAZI
Na HERIETH MAKWETTA
'UGUMU
wa Maisha ni Kipimo cha Akili'. Huu ni usemi uliozoeleka katika maisha
ya kijamii hasa kwenye miaka ya sasa ambapo hali ya uchumi imekuwa
ikizidi kuwa ngumu.
Katika
ugumu wa maisha huo kuna walioshindwa kabisa kujikwamua hadi kukata
tamaa. Lakini kuna ambao wameutumia ugumu huo kutafuta namna ya
kujikomboa, ndiyo wanaozungumzia kwenye usemi huu.
Mmoja
wa watu hao ni mtangazaji ambaye pia ni Mmiliki wa Local Media
Entertainment, kampuni inayoendesha vipindi vya televisheni vya
'Wanawake Live' na 'Bongo Movie', vinavyorushwa na Kituo cha EATV,
mwanadada Joyce Kiria.
Utumwa
pasipo malipo sahihi na kutokuwa na uhuru wa maamuzi, vilikuwa sehemu
ya maisha yake kwa muda mrefu. Ilikuwa ni baada ya kumaliza elimu yake
ya msingi.
"Unajua
natoka katika familia ya hali ya chini, hivyo nilipomaliza Darasa la
Saba sikuwa na namna ya kuendelea na masomo," anasema.
"Nilianza kwa kufanya kazi za ndani za u-hausigeli, nilifanya kazi hii kwa miaka miwili. Sikuifurahia sana.
"Baadaye
niliona nisonge mbele, niliiacha kazi hiyo na nikajiunga katika genge
la mama ntilie, nilifanya kazi hapo kwa muda mpaka nilipoamua kuanza
kuchoma chapati."
Hata
hivyo anasema hakudumu na kazi hiyo kwani hakuwa akipatana na moto
hivyo akatafuta kazi katika kiwanda cha mablanketi, Chang'ombe jijini
Dar es Salaam.
"Nikafanya
kazi kwa muda pale lakini baadaye nikapata nafasi ya kazi katika duka
moja Kariakoo, jijini Dar es Salaam, hapo ilikuwa tayari imefikia mwaka
2000," anaongeza.
"Niliendelea na kazi yangu na baadaye nilipata mtaji wa kuniwezesha kufungua biashara yangu."
Anasema
alianza biashara zake rasmi kwa kupigisha simu katika vibanda vidogo,
mtaji ulikua na baadaye alifungua duka la vifaa vya shule na mapambo,
lakini baadaye akairudia biashara ya nguo.
"Baada
ya kufanikiwa kukuza mtaji wangu, niliingia tena katika biashara ya
nguo, na nikaanza kununua nguo za jumla kutoka Dubai, Falme za Kiarabu,"
anasema.
"Siku
moja nikaenda na kununua nguo mwenyewe huko Falme za Kiarabu. Nilirudi
na kuona nguo hizo zimejaa sana Kariakoo na bei yake ipo chini, hapo
ndipo mtaji wangu ukafa au kwa maneno mengine nifilisika."
Anasema
baada ya kushindwa biashara akaamua kumwona, Amina Chifupa (sasa
marehemu) ambaye alikuwa mteja wake wa nguo na kumweleza shida yake.
"Amina
ambaye wakati huo alikuwa anafanya kazi redio ya Clouds akanishauri
nianze utangazaji kwani aliona nina kipaji, hivyo nilianza kazi hiyo
pale Clouds mwaka 2006. Mwaka 2008 nikaolewa," anasema.
KUVUNJIKA KWA NDOA YA AWALI
Joyce, ambaye sasa ni mke halali wa Henry Kilewo, ndoa yake ya kwanza ilikuwa mwaka 2008 alipooana na Nelson Joshua 'DJ Nelly'.
"Muda
mfupi baada ya ndoa nikaanza kuonja machungu yake, niliishi maisha
ambayo sikuchagua, hii ilikuwa ni baada ya kuolewa," anasema.
"Niliamua
kuachana na mume, unajua ilifikia hatua nilihisi ningeweza hata
kuwekewa sumu katika chakula, yalikuwa ni maisha ya chuki.
"Hapo
ndipo ukawa mwanzo wa kuyajua mengi ambayo niliamua rasmi kuanza
kuyafanyia kazi nikiwa kama mwanamke niliyejitolea kutetea haki za
wanawake."
Anasema alianza kwa kudai talaka ambayo ilikuwa ngumu kutolewa kwani ndoa aliyofunga ilikuwa ni ya Kikristo.
"Nilifanikiwa
kupewa talaka yangu na hapo ndipo ukawa mwanzo wa kuanzisha kipindi cha
Wanawake Live nikiwa na dhamira ya kweli ya kutetea Haki za Wanawake.
WITO WAKE KWA JAMII
Joyce ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Kilimanjaro, anasema tatizo lililopo hapa nchini ni mfumo dume, ambao umekithiri.
"Mwanaume
anasahau kutunza familia yake na kutokomea kusikojulikana, kwa sababu
ya uchumi mdogo familia yake inaingia kwenye taabu, hali hii haivumiliki
na ndiyo mwanzo wa kuvunjika kwa ndoa nyingi," anasema.
"Pia
changamoto za kimaisha ni nyingi, wapo wanawake wenye kipato, lakini
kutokana na mfumo dume wanalazimika kuacha kila kitu kikiwa chini ya
waume zao ambao baadaye huwasaliti."
Anasema
kupitia kazi yake ya sasa amepania kutoa elimu ya kutosha kwa jamii ili
iachane na na mfumo huo kuweza kutoa haki sawa kwa wote.
Habari hii kwa hisani ya gazeti la Mwanaspot.
Tuesday, 22 May 2012
Monday, 21 May 2012
NI MIAKA 16 TANGU MELI YA MV BUKOBA IZAME.
MELI YA MV BUKOBA
Historia
imewekwa leo na Flaviana Matata alipokabidhi msaada wa maboya (life
vests) 500 kwa Shirika la Meli la Taifa (Marine Services Co Ltd) kama
sehemu ya kumbukumbu ya MV Bukoba - ambapo ni miaka 16 tokea meli hiyo
ilizame na kuua watu takriban 1,000 akiwa pamoja na mama yake Flaviana .
MUNGU AZIWEKE ROHO ZA MAREHEMU WOTE MAHALA PEMA PEPONI,NA PIA MUNGU AWAPE NGUVU WOTE AMBAO WALIPOTEZA NDUGU ZAO KATIKA AJALI HIYO.
Thursday, 17 May 2012
GET WELL SOON MOM.
Kwanza poleni kwa kuwa kimya kwa siku kadhaa,ukweli ni kuwa mama yangu anaumwa alipata stroke wiki tatu zilizopita hivyo hata hamu ya kukaa na kuandika chochote ilipotea kabisa.
GET WELL SOON MY BEAUTIFUL MOM will see you soon.
GET WELL SOON MY BEAUTIFUL MOM will see you soon.
R.I.P DONNER SUMMER.
Donna Summer ,Queen of Disco,dead at 63 after secret cancer battle.
Family: Summer with her husband Bruce Sudano and their daughter Brooklyn in 2003. The couple also had another daughter together, Amanda. She had a daughter, Mimi, from a previous marriage
Family: Summer with her husband Bruce Sudano and their daughter Brooklyn in 2003. The couple also had another daughter together, Amanda. She had a daughter, Mimi, from a previous marriage
Monday, 7 May 2012
BIG BROTHER AFRICA 7 PARTICIPANTS FROM TANZANIA
Julio |
| Age | 27 | |
| Hometown | Tanzania | |
| Occupation | Manager | |
| Biography |
|
| Age | 28 | |
| Hometown | Tanzania | |
| Occupation | Saleswoman | |
| Biography |
|
ARM RECORDS.
ARM RECORDS ni studio iliyokuja kufanya mabadiliko ktk gem ya muziki wa kisasa tunajishughulisha na uandaaji(production) wa nyimbo aina zote kasoro bolingo
tunapatika
maeneo ya y/vituka tunatazamana na shule ya msingi y/vituka
unakaribishwa sana ktk hizo picha huyo jamaa aliyeweka nywele breach ni
kgt wa g2 na huyo mwingine ni kabo p ndie producer wetu hapa ni mie ndio
manager wa studio muda si mrefu utasikia ngoma.
NIMETUMIWA NA ADAM MZEE.
Wednesday, 2 May 2012
LINAH in DOWNTOWN NYC - U.S TOUR
She performed several of her hits but at this point most wanted MDUARA.
Great people, great night and to my amazement I stayed low key this time.
Artist AJ Ubao and NY's own Dr. Ebra on stage showing love n support
When
I say everyone I mean everyone had a crazy good time as we all aspired
to stay up till dawn on this night to Welcome Linah to our city and
temporary home (Bongo is #1)
PICHA NA MAELEZO NIMETUMIWA NA Growing Up African Blog.
Subscribe to:
Posts (Atom)






















