Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Sunday, 31 January 2010

Unashangaa Nini sasaaa?


Hii sasa kali,mbuzi akionyesha ushirikiano wa hali ya juu katika kuhakikisha wanafika mahali waendako....It`s real cool.

Saturday, 30 January 2010

Mke wa waziri wa Afrika Kusini akamatwa!

Mke wa waziri wa masuala ya kijasusi wa Afrika Kusini amekamatwa kwa madai ya kuhusika na biashara ya dawa za kulevya.
Sheryl Cwele, mwenye umri wa miaka 50, mke wa Siyabonga Cwele, amefikishwa mahakamani akishtakiwa kwa jaribio la kuingiza cocaine nchini Afrika Kusini.

Bi Cwele ameshtakiwa kwa kumtumia mwanamke mmoja kuchukua dawa hizo Uturuki na kumwajiri mwanamke mwengine kuzichukua kutoka Brazil.

Amewekwa rumande mpaka dhamana yake itakaposikilizwa katika wiki moja ijayo.

Bi Cwele anakabiliwa na shutuma hizo pamoja na Frank Nabolis, raia wa Nigeria aliyekamatwa Afrika Kusini mwezi Desemba.

Wednesday, 27 January 2010

Bongo Inazidi Kung`ara!!


So far so good, bongo Yetu inazidi kung`ara na majengo Mapya, jengo hili lipo katika makutano ya morocco ambako zamani kulikuwa na jengo la Gogo hotel.Inapendeza kwa kweli.Picha kwa hisani ya Ray The Greatest.

Tuesday, 26 January 2010

Ujenzi wa Haiti kuchukua mwongo mmoja !


Itachukua muongo mmoja kukarabati nchi ya Haiti ambapo kulitokea uharibifu mkubwa uliosababishwa na tetemeko la ardhi.
Hiyo ni kauli ya waziri mkuu wa Canada Stephen Herper wakati kongamano la siku moja la wafadhili wa kimataifa mjini Montreal kujadili mustakabhali wa kisiwa hicho.

Akizungumza baada ya kongamano hilo kumalizika waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton amesema wafadhili hawapaswi kuwaachia wananchi wa Haiti jukumu la kuijenga upya nchi yao.

Naye waziri mkuu wa Haiti Jean Max Belerieve amewakumbusha wafadhili kuhusu mahitaji muhimu ya nchi hiyo ikiwa ni pamoja na vitanda laki mbili na huduma za afya na matibabu kwa takriban watu laki nne.

Mkasa wa tetemeko la ardhi lenye kipimo cha saba kwenye vipimo vya Richer ulisababisha vifo vya takriban watu laki mbili na kuiacha Haiti mojawapo wa nchi masikini kabisa duniani ikikabiliana na uharibifu wa kiwango cha juu.

Kongamano kuu la wafadhili litafanyika mwezi Machi nchini Marekani ili kujadili zaidi mstakabhali wa Haiti.

Monday, 25 January 2010

Wanaume Wa kichina Hatarini kukosa Wenza!!


Mwishoni mwa miaka ya 1970 China ilipitisha sheria ya kuzaa mtoto Mmoja katika kila familia, lengo lilikuwa ni kupunguza idadi ya watu nchini humo.Na familia nyingi walipendelea mtoto wa kiume wakiamini akikua atawasaidia wazazi wake tofauti na mtoto wa kike,wazazi walichofanya ikionekana mimba ni ya mtoto wa kike basi mimba hiyo ilitolewa haraka.Matokeo yake sheria hiyo imepelekea kuwa na wanaume wengi zaidi kuliko wanawake kwa sasa nchini China.Inasemekana katika miaka 10 ijayo wanaume millioni 24 wa Kichina huenda wakajikuta wanakosa wanawake wa kuwaoa...Hivi thamani ya mtoto wa kike itakuja onekana lini? katika mabara haya mawili Asia na Africa.

Friday, 22 January 2010

Nawatakia Weekend Njema Wote!!


Wenye kuendesha Magari Msinywe Pombe na kuendesha magari.....Ushauri wa bureee.
Love you all.

Thursday, 21 January 2010

Jamani Hii ni Haki Kweli!!


Tunakoelekea sasa siko kabisaaa,Yaani mwili wa Mtoto unatumika kwa Matangazo?....Poor baby.

Wednesday, 20 January 2010

Ghasia zadhibitiwa Nigeria!!

Jeshi la Nigeria limesema limechukua udhibiti wa mji wa Jos,ambapo mapigano ya hivi karibuni kati ya waislamu na wakristo yalisababisha vifo vya watu kadhaa.
Luteni Kanali Shekari Galadima ameiambia BBC kuwa mji "uko shwari" wakati jeshi likihakikisha kuwa amri ya kutotoka nje kwa muda wa saa 24 inatekelezwa. Amesisitiza kuwa hakutakuwa na ghasia tena.

Lakini mwandishi wa BBC katika eneo hilo anasema ghasia sasa zimezidi hadi katika mji wa Pankshin, kilomita 100 kutoka Jos.

Makundi ya kutetea haki za binaadamu yanasema takriban watu 200 wanaaminika kufariki dunia tangu Jumapili.

Mji wa Jos umekumbwa na mapigano ya kidini kwa takriban muongo mmoja uliopita.
Chanzo BBC.

Tuesday, 19 January 2010

Young Tanzanian Entrepeneur!!


Emelda Mwamaga ni mkurugenzi na mmiliki wa Bang Magazine, ni miongoni mwa mabinti wajasiriamali Tanzania ambao wanamafanikio Makubwa. Emelda ni mfano wa kuigwa hususani kwa sisi vijana.Blog hii ya Strive For Life inakutakia kila raheri katika safari yako ya ujasiriamali.

Sunday, 17 January 2010

THE UGALIIIIIIZI!!


Hili nguna linaenda kwa mboga ya aina yeyote halina ubaguzi,Kwa mrenda sawa,maharage poa,nyama ya kuku,ng`ombe twende.Mimi linashuka sawa sawa na nyanya chungu zile za uchunguuuuu kabisaaaa! zikichanganywa na nyama ya ng`ombe utamu wake unausikilizia hadi kisogoni.....Ooooh i badly miss this thing.

Thursday, 14 January 2010

Brad and Angelina Donate $1 Million to Haiti Quake Relief


Brad Pitt and Angelina Jolie’s foundation is contributing $1 million to the emergency medical operation responding to the devastating 7.0-magnitude quake in Haiti.

“It is incredibly horrible to see a catastrophe of this size hit a people who have been suffering from extreme poverty, violence and unrest for so many decades,” says Jolie.

Adds Pitt: “We understand the first response is critical to serve the immediate needs of countless people who are now displaced from their homes, are suffering trauma, and most require urgent care.”

Wednesday, 13 January 2010

TETEMEKO LA ARDHI LAIKUMBA HAITI!!


Maelfu wanahofiwa kufa kufuatia tetemeko hilo lililotokea nchini Haiti ambalo lilikuwa la kipimo cha 7.3 katika vipimo vya Ritcher.
Ripoti zinasema uharibifu mkubwa umetokea katikati mwa mji mkuu wa Port-au-Prince. Baadhi ya majengo yaliyoharibiwa vibaya ni ikulu ya rais na hospitali moja mjini humo.

Msemaji wa umoja wa mataifa mjini New York Martin Nesirkyo amethibitisha kuwa ofisi za umoja wa mataifa mjini Port-au-Prince zimeharibiwa. Amesema pia kuwa idadi kubwa ya watu wamezikwa chini ya vifusi na wengine kufa au kujeruhiwa.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Hilary Clinton amesema Marekani tayari imeanza kutuma misaada ya dharura.

Tuesday, 12 January 2010

Ama Kweli Life Is Not fair,


Kadri siku zinavyozidi kwenda tofauti ya maisha ya Mtanzania inazidi kuwa kubwa,aliye masikini anazidi kuwa masikini zaidi na aliye tajiri anazidi kuwa tajiri zaidi.Lini yule masikini atafurahia matunda ya nchi yake? Lol.... this make me sick.I quote some words from Bob Marley he said * How can you be sitting there and telling me that you care when every time i look around the people suffering in every way*. Is this what you call maisha bora kwa kila Mtanzania?

DOLLARISATION OF THE SHILLING

Saturday, 9 January 2010

Wish You Great Weekend With Lots Of Love!


Drive safetly,Drink little,Dont break the rules,and for those who are turning age this weekend Let me wish you HAPPY BIRTHDAY.

Friday, 8 January 2010

Uganda Kutowanyonga Mashoga!


Mswada mpya nchini Uganda unaotoa adhabu kali kwa wapenzi wa jinsia moja unatarajiwa kuondoa kipengele cha hukumu ya kifo dhidi ya watu hao.
Wabunge wa chama tawala hata hivyo wamesisitiza kwamba mswada huo ambao unapendekeza adhabu kali utawasilishwa mbele ya bunge hivi karibuni.

Baadhi ya nchi za magharibi zimepinga mswada huo ikiwemo Marekani.

Sweden imetishia kuondoa msaada kwa Uganda ikiwa mswada huo utaptishwa kuwa sheria.

Wednesday, 6 January 2010

PIGGE AMERUDI TENA KUJIVINJARI PALE PALE ALIPONUSURIKA KUFA


Pigge Werkelin,akiwa na mke wake Monica na watoto Nicole 17,Wilda 2 na wa mwisho miezi 5.
Ikiwa ni miaka 5 toka maafa ya Tsunami kutokea ambapo maelfu ya watu walipoteza maisha miongoni mwao wakiwa ni Waswidish 500 walipoteza maisha nchini Thailand,huyo jamaa hapo juu yeye alinusurika kufa lakini alipoteza Mke na watoto wawili wa kiume.Baada ya kunusurika kufa akaona yaliyopita sindwele akaamua kuoa tena na kubahatika kupata watoto wawili tena hao wadogo,huyo binti mkubwa ni wa mwanamke.Licha ya kunusurika kufa huyu jamaa amerudi tena kujivinjari na familia yake mpya kwenye ile ile beach ambayo aliyopoteza wapendwa wake na yeye kunusurika.

Monday, 4 January 2010

Rais Zuma Kuoa Mke wa Tano!


Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma atafunga ndoa ya tano baadaye leo.
Harusi yake itafanyika kuzingatia mila na desturi za jamii ya Zulu ambapo Thobeka Stacey Mabhija atakuwa mke wa tatu wa Zuma.

Wake wengine wawili wa Zuma Sizakele Khumalo-Zuma na Nompumelelo Ntuli-Zuma sharti washiriki sherehe ya leo ili kumkubali mke mwenza wao.

Rais Zuma pia amesha mposa mwanamke mwingine na tayari amelipa mahari.

Waandishi habari wamesema imani ya Zuma kuwa na wake wengi imeigawanya jamii Afrika Kusini.

Baadhi wanamuunga mkono huku vijana wengi wakisema desturi hiyo imepitwa na wakati.

Mmoja wa wake wa Zuma Kate Mantsho-Zuma alifariki dunia na rais huyo alitengana na waziri wa mambo ya ndani wa Nkosazana Dlamini Zuma.

Sunday, 3 January 2010

RIHANNA`S NEW YEAR`S RESOLUTIONS


Ni jambo la kumshukuru Mungu unapopata nafasi ya kuweza kuuona mwaka Mpya kwani ni wengi walitamani kuuona ili waweze kutimiza malengo waliyokuwa wamejiwekea kuyatimiza kwa mwaka huu lakini hawakuweza,so sisi tuliopata bahati ya kuuona mwaka natumaini tuna malengo na mikakati ya kutekeleza mwaka huu 2010 and this is what we call new year resolution,The R&B singer Rihanna has made several new years resolutions that she intends to keep,She said: “I want to stop shopping, being late, start waking up early, stuff like that.

Saturday, 2 January 2010

Mshukiwa wa Al-Shabab ajeruhiwa Denmark

Polisi nchini Denmark wamempiga risasi na kumjeruhi Msomali kwenye nyumba ya mchora katuni aliyechora katuni zenye utata za Mtume Mohammed.
Polisi wamesema mtu huyo ambaye ana uhusiano wa karibu na kundi la kiislam nchini Somalia la Al-Shabab, ameingia nyumbani kwa Kurt Westergaard katika mji wa Aarhus, akiwa amejihami kwa kisu na kutishia kumwua mchora katuni huyo.

Polisi walidokezwa tukio hilo kupitia ala za electroniki zinazotoa ishara ya hatari, na kisha kumpiga risasi mtu huyo mara mbili.

Inadaiwa kuwa mtuhumiwa anashukiwa kuhusika na vitendo vya kigaidi katika nchi za pembe ya Afrika.

Bw Westergaard amepokea vitisho kadhaa vya kumwua tangu kuchapisha katuni hizo kwenye gazeti miaka minne iliyopita, ambazo Waisamu wengi walizichukulia kama fedheha na kejeli ya imani yao.