Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Saturday, 31 July 2010

MDAU ENJOY YOUR WEEKEND TO THE FULLEST.

Waendesha magari endesheni kwa kuzingatia sheria za barabarani,wanywaji wa pombe kunyweni kiasi..,kuleni kiasi msije vimbiwa.Wababa mkae majumbani na wake zenu na wamama pia kaeni nyumbani na familia zenu.May God bless you all,am outtttttt.

Friday, 30 July 2010

JANA ILINYESHA MVUA KUBWA HAPA SWEDEN.

Kwa mujibu wa wenye Nchi wanasema haijiwahi kunyesha mvua kubwa kama hii kwa miaka mingi sana.
Maji yalikuwa kila mahali watu walilazimika kuvuka na mitumbwi,...mwaka huu nafikiri kila kitu kilikuwa zaidi ya kawaida, wakati wa winter kulikuwa na snow nyingi kuliko kawaida,summer jua lilikuwa kali sana utafikiri lile la kwetu,na sasa mvua ndiyo hiyo.Wataalam wa hali ya hewa labda wanaweza kutusaidia mabadiliko haya husababishwa na nini.

Wednesday, 28 July 2010

SOON NITAVUNA NYANYA.

Nilipanda kama utani vile wengine walifikiri ni maua tu,siamini kama zimekuwa hivi.
Nilipopanda kila mtu alikuwa akicheka na kusema si rahisi kupata nyanya kutokana na hali ya hewa ya hapa,pili nimepanda kwenye makopo tatu jua lenyewe la kubahatisha,lakini kila anayeziona sasa anashangaa na wengine wanataka wakajaribu kupanda makwao.
....nategemea kuvuna muda si mrefu.

Tuesday, 27 July 2010

HII KWAKO WEWE ULIYEKATA TAMAA YA KUOLEWA AU KUOA.


Henry Kerr 97 na Valerie Berkowitz 87 raia wa uingereza huenda wakawa ni watu waliovujunja record kwa kuoana wakiwa na umri Mkubwa(vikongwe) mmmmh kweli mapenzi hayana umri.Kilichonifanya niweke hii post ni kuwapa faraja wale wote waliokata tamaa ya kuolewa au kuoa kutokana na umri wao,nina rafiki yangu yeye ana miaka kama 35 yeye ameshakata tamaa kabisaaaa ya kuolewa kwa kuwa anaona umri wake umeshasogea sana na kila anayekuwa naye anamchezea tuu alafu anatokomea.... i always encourage her It is never too late to get married.

Sunday, 25 July 2010

Aomba apunguziwe mpaka bure......Cheka unenepe.


Jamaa mmoja toka bushi aliingia mjini na kufikia kwa ndugu yake, katika tembea tembea yake alimtembeza sehemu zote muhimu kama Kariakoo mtaa wa Kongo na Soko la Karume.
Baada ya kulifahamu jiji kidogo, siku moja alimuomba ndugu yake pesa aende akanunue vitu. Ndugu yake baada ya kumpa pesa, alimueleza;

“Unajua mjini wanauza nguo kulingana na muonekano wako, sasa mtu akikuuzia nguo usikubali moja kwa moja, komaa naye akupunguzie lazima utanunua kwa bei ndogo.”
Baada ya maelekezo jamaa aliingia mitaa ya Mchikichini na kukutana na jamaa anauza viatu.

“Viatu bei gani?”
“Elfu 22.”
“Aah, nipunguzie bwana.”
“Leta basi ishirini.”
“Nipunguzie bwana.”
“Wewe mnunuzi kweli?”
”Ndiyo.”

“Basi leta 15.”
“Nipunguzie bwana.”
“Bei ya mwisho 10.”
“Nipunguzie bwana.”
“Kila bei nikupunguzie, basi chukua bure.”

“Aah, nipunguzie bwana.”
Muuza mitumba aliamini yule jamaa hakuwa mzima anapoomba apunguziwe hata bure.

Thursday, 22 July 2010

HII NDIO BONGO DAR ES SALAAM.


Bongo Dar es salaam ni tambarare popote pale ni jalala,Angalia lundo la takataka lilivyotulia pembeni ya barabara....Lawama tumtupie nani? jiji (serikali) kwa kuwa hawajaweka sehemu maalumu za kutupa takataka? au hao watu wanaotupa takataka hapo kwa makusudi?.Au ndio tunasubiri mpaka kipindupindu kitupindue ndio tutaanza kuchimba mashimo.

Monday, 19 July 2010

Madhara unayoweza kupata ukivumilia shida kwa muda mrefu.


BILA shaka wengi tumeambiwa mara nyingi kauli hizi “Vumilia tu ndugu yangu” na tukakubaliana na ushauri huo na kuendelea kunyanyaswa, kuonewa na kuumizwa na mambo mabaya wanayotutendea wenzatu katika maisha, bila kujua kuwa uamuzi wa kuvumilia shida una madhara makubwa kwetu.

Takwimu zinaonesha kuwa wana ndoa na wapenzi wengi wanaishi maisha ya uvumilivu usiohitajika, ambao umezifanya familia nyingi kukumbwa na matatizo, yakiwemo matukio ya watu kuua, kujiua au kuwadhuru wengine.

Kisa kikubwa kinachochangia haya yote ni uvumilivu usiokuwa na sababu ambao watu wamekuwa nao wakiamini kuwa shida na uvumilivu ni vitu vinavyokwenda pamoja kwa wakati wote.

Elimu ya Ufahamu na Nafsi inakataa kanuni ya uvumilivu usiokuwa na sababu kwa vile humfanya mhusika aishi nje ya matakwa yake na hivyo kuathiri mfumo wa akili yake na kuvuruga kinga ya mwili, jambo linaloweza kumsababishia mhusika magonjwa ya moyo au bumbuazi.

Wengi kati ya watu wanaoshambuliwa na magonjwa ya moyo nyakati hizi wanatajwa kusababishwa na msongo wa mawazo unaotokana na msukumo wa lazima wa kimaisha wanaokabiliana nao kwenye ndoa, familia, jamii na maeneo yao ya kazi.

Kama hilo halitoshi, vifo vingi vya ghafla, magonjwa ya kudumu yenye tiba wanayosumbua watu yanaelezwa kuchangiwa na hali ya mtu kukata tamaa ya kuishi itokayo ndani.

Usomapo makala haya unaweza kuyathibitisha kwa kufanya uchunguzi wa kuwatembelea wagonjwa wa muda mrefu na kuwauliza historia za maisha yao, utabaini wamekuwa kwenye uvumilivu wa dhiki.

Niandikapo madhara ya uvumilivu, simaanishi watu wasivumilie shida zao, bali katika kila uvumilivu lazima ziwepo sababu za msingi.
Ikiwa mtu anateswa na mume au mke wake lazima ajiulize ana sababu gani ya kuvumilia, na je sababu hiyo ni ya msingi au anatumikia mateso yatakayomuua hatimaye?

Ikiwa mtu atakuwa anavumilia bila kuwa na sababu za msingi hawezi kukwepa madhara niliyoyataja hapo juu, na bahati mbaya wakati mwingi madhara hutokea bila mhusika kujua chanzo.

Ushahidi wa kauli “nilidondoka tu, nilipopimwa nikaambiwa nina presha” upo mwingi, na watu wamekuwa wakiambiwa “moyo wako umetanuka,” kilichotanua moyo hakijui, kumbe ni msongo wa mawazo uliotokana na uvumilivu wake usiokuwa na sababu.

Kitaalamu sababu ya mtu kuvumilia jambo ndiyo ngao ya madhara, kwani hakuna tatizo mtu kuvumilia maumivu wakati wa kujifungua huku akiamini kuwa baadaye atapata mtoto.

Hii ina maana kuwa, lazima mtu afahamu anavumilia kwa faida gani, atapata nini kuishi na mwanaume mlevi anayesumbua kwa tabia zake za usaliti? Kuna faida gani kuvumilia manyanyaso ya bosi kazini au utapata nini kuishi na ndugu anayekutesa? Je, ni haki kwako kuishi maisha ya utumwa?

Kama hakuna faida za msingi, ukiendelea kung’ang’ania maisha ya mateso kwa madai ya kuvumilia, huwezi kushinda mashambulizi yake, ipo siku usiyoijua utajikuta umepata tatizo baya litakalokuweka pabaya zaidi, ambapo hutaweza kupavumilia hata kidogo.

Nimalizie kwa kuweka wazi lengo langu la kuacha uvumilivu usiokuwa na sababu kwa kumtaka kila mtu mwenye shida awe na sababu ya kuivumilia. “Nitavumilia mateso haya, baada ya mwaka mmoja nitamaliza shule na kupata cheti kitakachonisaidia kwenye maisha yangu.” “Nitavumilia mpaka nipate kazi nyingine.”

Nia yangu ni kumfanya kila mvumilivu kuwa na sababu za msingi, wasiokuwa nazo ni bora wakaondokana na uvumilivu wao na kutafuta maisha mengine mbali na hapo wanapopavumilia.
Source Globalpublishers.

Sunday, 18 July 2010

BRAND NEW VIDEO FROM KIDUMU FT LADY JAYDEE!


Watu wawili wenye vipaji na sauti za kumtoa nyoka pangoni walipokutana na kuamua kuingia studio kutengeneza wimbo wa "NITAFANYA" na hatimae video.....Nimependa mengi kwenye hii video,kwanza wote wamependeza,pili sauti zao ndio balaa,tatu ujumbe uliomo,na nne vile Lady JayDee alivyoonyesha hisia utafikiri kweli yamemkuta.

Sunday, 11 July 2010

JAMANI NJAA HAINA ADABU NA HAICHAGUI MTU.

Bibi akiwa amefungasha mzigo wa Bangi, mwenyewe alikuwa amejiandaa tayari kwenda kafanya biashara lakini bahati haikuwa yake wajanja wamemnasa.
Polisi wakimpekuwa bibi mwenye umri wa miaka 94 alikamatwa maeneo ya Nogales Arizona akiwa na bonge la mzigo wa bangi....Swali ni je kweli huyu bibi hiyo biashara ilikuwa ni ya kwake ?au wajanja walimtumilizia wakiamini bibi kama huyo hawezi kushukiwa kama anaweza fanya biashara kama hiyo? Mie naona she is toooooo old for that,....na kama ilikuwa ni biashara yake then the World is coming to an end.

Friday, 9 July 2010

WONDERFUL FRIDAY IS ALL I CAN SAY.....



And while enjoying your friday i just want you to read this......
First i was dying to finish my high school and to start college
And then i was dying to finish college and start working.
Then i was dying to marry and have children
And then i was dying for my children to grow old enough
so i could go back to work.
But then i was dying to retire
And now iam dying........
And suddenly i realized
i forgot to live.


And remember....
To make money we lose our health,
And then to restore our health we lose our money.......
We live as if we are never going to die,
And we die as if we never lived......


Please do not let it happen to you,
Appreciate your current situation
and enjoy each day of your life .

Wednesday, 7 July 2010

HAWA NDIO VIJANA WALIOJITOKEZA KUGOMBEA UBUNGE 2010.

Shy-Rose Bhanji (CCM)
Nakaaya Sumari (CHADEMA)
Joseph Mbilinyi( a.k.a Mr 2) (CHADEMA)
Januari Makamba (CCM)

Inaleta faraja kuona vijana wameamka na kuwa na machungu na Taifa Letu La Tanzania ambalo linaelekea kupotea kutokana na uongozi mbovu uliopo sasa, haikuzoeleka hivi miaka kadhaa iliyopita kuona kijana anajitokeza kuwania nafasi yoyote ya Uongozi, sijui ilikuwa ni uoga au kutojimani.Binafsi naamini endapo watapata nafasi wataleta mabadiliko makubwa Tanzania.

Thursday, 1 July 2010

USHAWAHI KULA MTORI WEYE?


Nilikuwa na rafiki yangu mchaga enzi hizoooo! yeye bwana ilikuwa kila ukimtembelea kwake msosi ni Mtori,mwenyewe alikuwa akichanganya viazi,ndizi,nyama na vikolombwezo vingine kibao hata majina sikumbuka,ukianza kula utamu wake unausikilizia hadi kisogoni.I miss you so much girl hope to see you sometime in future.