Pages

Subscribe:

Ads 468x60px

Monday, 30 August 2010

UJUMBE NA UMFIKIE MHUSIKA!!!


"UTAKULA ULIKOPELEKA MBOGA"

PALE USHOGA UNAPO KUWA SI USHOGA TENA….!!!!


Amekuwa rafiki yako kwa mda mrefu na mmeshuka na kupanda milima wote mkiwa na mshikamano. Lakini katika maisha yenu yote hamjawahi kuwa na mikwaruzano.

Sasa mmejikuta urafiki wenu upo hatarini kusambaratika chanzo kikubwa ni kutoelewana katiyenu juu ya maswala fulani. Pale hasira zinapo teka akili zenu hali yakupatana inazidi kupotea na dalili za urafiki wenu au ushoga ndio unazidi kuwa katika hati hati ya kufutika.

Chunga sana kabla hamjaamua kufutiana namba za simu, na kusonyana wakati mnapishana mitaani kaeni chini na mjaribu kuyafikiria haya na kuyafanyia kazi yafuatayo.

Tafakarini chanzo cha ugomvi wenu: Tafuta mahali ambapo pametulia nauanze kutafakari nini kilichofanya nyie mfikie hapo mlipo sasa. Jaribu kujikumbusha majadiliano mlio yafanya mpaka yaka sababisha ugomvi wenu. Angalia kama mlicho kizungumza sikiu hiyo ndio chanzo au kuna vitu vingine vimejificha?

Tengenezeni Mipango: tambueni nini mtakacho kizungumza kabla hamjakutana tena. Msikubali maongezi yenu yakawaingiza kwenye ugomvi kwa mara ya pili. Cha muhimu zingatieni maneno ya busara yatakayo wafikisha katika suluisho.

Jitayarishe Kuomba msamaha: Kama utagundua ulifanya makosa basi kuwa tayari kuomba msamaha. Katika urafiki kuwatayari kukubali kosa, kwasababu mwanadamu anatabia ya kukimbia makosa.

Jaribuni kuzungumza point tu: Wakati wa kudiskasi ukiwa umewadia jitahidini kuanza na pointi zihusianazo na utatuzi wa ugomvi wenu.Bila kusahau mambo mlio yafanya pamoja wakati mkiwa katika urafiki mzuri hiyo itasaidia kurudisha kumbukumbu nzuri za urafiki...source Mohamed Dewji blog.

Saturday, 28 August 2010

LOVELY WEEKEND!


My lovely lil sis Tabby

And the big sis of course,together we wish you fabulous weekend...kwa mbaaali tumefanana eheee...We all have big eyes.

Thursday, 26 August 2010

YUPO KAZINI!


Watu wamemuamini MUGAMBO na kumkabidhi mali zao na usalama wao ,lakini jamaa kauchapa usingizi kama hayupo kazini vile..... Mwizi akija atajichukulia kila kilichopo kiulaiiini.Alafu silaha aliyokuwa nayo ni kirungu, sasa imagine limekuja jambazi na bastora sijui itakuwaje mmmmh.

Monday, 23 August 2010

WANAWAKE NA VIATU!


Inasemekana wanawake/wasichana wanapenda viatu kuliko wanaume/vijana na wanatumia pesa nyingi kwenye viatu, I mean mapenzi ya viatu sio mapenzi ya mwanamke na mwanaume).Utakuta mwanamke/msichana mmoja ana pair za viatu zaidi ya hamsini (50) na bado akipita dukani akaona kiatu kizuri atanunua kama hana hela yupo radhi akope,wakati mwanaume anaweza kuwa na pair mbili au tatu tuu za viatu na akaridhika kabisaa.I have to admit i also love shoes so so much... lakini sijafikisha hizo pair hamsini mweeeeeeee.


CHEKA UNENEPE.

Msukuma mmoja alibahatika kwenda zake Uingereza, baada ya kufika alishangaa uzuri wa mji na majengo ya kushangaza.

Ili akirudi Tanzania awakonge wenzake kila alichokiona alitaka kujua kinamilikiwa na nani. Cha kwanza kuuliza kilikuwa kujua uwanja ule wa ndege unamilikiwa na nani. Alimuona Mzungu mmoja amesimama alimfuata na kumuuliza.

“Eti uwanja huu wa ndege ni wa nani?”
“Speak English,” Mzungu hakumuelewa na kumuomba azungumze Kiingereza.

Jamaa baada ya kuelezwa vile aliondoka akiamini anayemiliki ule uwanja ni speak English. Alipoondoka pale alikwenda hoteli moja kubwa na kuulizia ile ni ya nani, aliyemuuliza kwa Kiswahili hakumuelewa alimjibu.
“Speak English.”

Kila kona alielezwa vile, basi jamaa aliporudi Tanzani aliamini Speak English ndiye tajiri mkubwa nchini Uingereza. Kila kona aliwaeleza jinsi kila kona alipouliza watu kuhusu mmiliki wa vitu vya thamani aliambiwa Speak English.

Watu walimcheka na kumueleza Speak English siyo tariji bali walimueleza azungumze Kiingereza kwa vile walikuwa hawamuelewi akizungumza kiswahili.
Mmh, hii kali kujua lugha nako raha.

Saturday, 21 August 2010

MKULIMA BORA WA MWAKA!

ulikuja upepo wa ajabu ukaziangusha nyanya,...nikaziinua na kuzifunga kamba kwa unyonge huku nikiwa nimekata tamaa ya kuuendelea kukua.
What a best mkulima, ona manyanya yanavyopendeza hahahaaa

Furaha ya mkulima siku zote ni kuvuna kile alichopanda,nami leo nina furaha ya ajabu kuvuna mazao yangu (nyanya) sikutegemea kama zingekuwa hivi...i mean zina afya, zinapendeza na ziko tayari kuvumwa.Sina budi kujiita mkulima bora wa mwaka.

Thursday, 19 August 2010

Vuvuzela yaingia kwenye kamusi ya Kiingereza


Mashindano ya Kombe la Dunia na hali ya kuyumba kwa uchumi ni mambo yaliyosababisha kujumuishwa kwa maneno mapya katika kamusi ya Kiingereza ya Oxford (Oxford Dictionary of English).

Vuvuzela, ni neno jipya, likiwa na maana ya chombo cha kupulizwa kilichotumiwa na mashabiki wa soka wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini.

Vile vile matatizo ya uchumi duniani yameongeza "toxic debt" - deni lenye uwezekano wa kutolipwa.

Kamusi hiyo - tofauti na nyingine ijulikanayo kama Oxford English Dictionary (OED) ilichapishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1998 - ina maneno mapya zaidi ya 2,000.

Inakusudia kuainisha mambo ya kisasa katika matumizi ya lugha ya kiingereza.

Toleo lake la tatu lilihusisha maswala ya mabadiliko ya hali ya hewa duniani.

Monday, 16 August 2010

MIUJIZA!



Bogota Colombia,ndege Boeing 737 (Colombian Airline)iliyokuwa na abiria 131 imeanguka na kumegekeka vipande vitatu ilipokuwa ikijiandaa kutua...cha ajabu ni mtu mmoja tu ndie amepoteza maisha kwangu mimi naweza ita ni muujiza...Mungu na ashukuriwe.

Sunday, 15 August 2010

Thursday, 12 August 2010

BONGO KILA MTU MWANAMZIKI.


Ama kweli Money Talks, Bongo ukiwa na pesa ya kuingia studio na kurecord tayari wewe ni mwanamziki,kipaji sio muhimu wala nini...Joti nae amejitosa kwenye ulimwengu wa Muziki na JIBWA KOKO.Video kwa msaada wa blog ya DJ CHOKA.

Plate Number za namna hii marufuku Sweden.

Wednesday, 11 August 2010

Lund University adjust the new admission rules.


After the criticism against new admission system for Swedish universities, which is seen as discriminatory against foreign students, Lund University will now make a special arrangement in order to improve the possabilities for students with foreign grades to get enrolled on their courses this fall semester
120 of the 1100 courses and programs will be affected and around 75 students are believed to get accepted at their desired courses this way according to the daily newspaper DN.

One of the problems in the brand new admission system is that students with foreign grades are in an admission group of their own. The reason for this is that Swedish students who have taken certain courses in high school get extra credits in order to stimulate high school students to choose these subjets. It is for example language courses and mathematics that the system wants to reward.

Foreign students can't get the extra credit since their high school courses are not always comparable and the standard is sometimes hard to analyse for Swedish universities. The foreign students would then have a disadvantage. That is why they created special admission groups for foreign students. The problem is that these groups might sometimes be so small that no one from the group gets into the course, even if they have top grades.

Tuesday, 10 August 2010

Simu yamchengua Msambaa!


Baada ya kutokea msiba huko Lushoto walimtuma ndugu yao mmoja kwenda kuwajulisha ndugu zake waliokuwa nje ya mkoa wa Tanga. Mtani wangu Msambaa aitwae Abdalahaman Shemaonge, alikwenda kwenye ofisi za shirika la simu hapo Lushoto. Baada ya kutoa namba aliandikiwa, aliunganishwa na mjomba wake Juma aliyekuwa akiishi Dar es Salaam.

Baada ya kuunganishwa mambo yalikuwa hivi:
Juma: Juma hapa, naongea na nani?”
Shemaonge: Shemaonge, ni Juma?”
Juma: Ndiyo, shikamoo mjomba.”
Shemaonge: Marahaba, yaani twasikilizana Lushoto na Dashalama?”

“Juma: Ndiyo mjomba, habari za huko?”
Shemaonge: Nakwambia siamini macho yangu, yaani twasikilizana, ama kweli huu ni waya kwa waya.”
Juma: Mjomba dunia ya teknolojia hii, unashangaa simu tu, mbona kuna mambo mengi ya kushangaza.”
Shemaonge: Haah,si hadithi hii? Sauti yako naisikia vizuri kabisa kama upo sikioni pangu, eeh kweli mzungu mwendawazimu.”

Shemahonge kwa kuishangaa simu alijikuta anamaliza dakika zote alizolipia bila kutoa taarifa ya msiba. Kweli ushamba mzigo.

Saturday, 7 August 2010

WARMLY WEEKEND !


My best female singer of all time in East Africa Lady Jaydee,jana ametimiza miaka kumi tokea aanze shughuli zake za Muziki, kapitia Mengi mpaka kufika hapo alipo but so far so good she made it hongera sana dada....Hapa akiwa ameshirikishwa na Ngoni kutoka Uganda wimbo unaitwa SIRIMBA I bet you gonna love it...I`m out will be back on Monday.

Friday, 6 August 2010

"Romani people are deported without legal reason"

Sweden deports Romani people without proper legal reason. This claims former Liberal People’s Party (Sw: Folkpartiet) chairman Maria Leissner, now chairman for the government’s committee on Romani issues.

So far this year, fifty Romani people have been deported because they were begging for money in the metro and other public places reports the Swedish radio. Begging is however not illegal in Sweden and many of them are EU-citizens and thus have the right to remain in another country in the union for three months anyway. The Stockholm police claim however that they are following the Swedish law when they deport foreign citizens who can not support themselves



Minister for Migration Tobias Billström says to the daily newspaper Dagens Nyheter (DN) that Romani people needs to support themselves in a reasonable way in order to stay. Begging in the metro is not such a proper way he claims. Billström says that every member state has to solve its minority problems in a way that improves the rights for the minorities
We can not solve Romania’s, Bulgaria’s or some other Eastern European country’s problem with the exposure of their Romani population by them moving from one country to another. It is not because people should be able to travel around begging that we have created the free movement in the EU he said to DN


Nyamko Sabuni.
Minister for Integration and Gender Equality Nyamko Sabuni and Minister for European Affairs Birgitta Ohlsson has writen a letter to the European commission in order to stress all member states responsibility for the Romani population
There are so many prejudices about Romani people. They are the only group in society that one can express things about and discriminate against without any one reacting says Sabuni to DN.

Thursday, 5 August 2010

Naomi Campbell kutoa ushahidi dhidi ya Charles Taylor


Mwanamitindo Naomi Campbell, anatarajiwa kutoa ushahidi katika mahakama ya jinai huko the Hague kwenye kesi inayomkabili rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor.

Bi Campbell inadaiwa alipokea almasi kutoka kwa rais huyo wa zamani kama zawadi mwaka 1997 -- ingawa amekanusha.

Bwana Taylor anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya kivita katika mahakama maalum kuhusu Sierra Leone huko the Hague, inadaiwa alimkabidhi Bi Campbell almasi kama zawadi mnamo mwaka huo akiwa nchini Afrika kusini kwa mwaliko wa rais mstaafu Nelson Mandela.

Hata hivyo Taylor amekanusha madai hayo na ndio sababu kuu ya bi Campbell kutakiwa kutoa ushahidi katika kesi hiyo.

Madai hayo pia yamesemekana kuwa sababu ya kesi dhidi ya Yaylor kwa vitendo vyake, wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika nchi jirani ya Sierra Leone.

Upande wa mashtaka ungetaka kuthibitisha kuwa bwana Taylor alihusika katika biashara ya kubadilishana silaha na kupewa Almasi zilizopatikana kutokana na vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sierra Leone

Tuesday, 3 August 2010

MBINU MPYA YA WIZI.


Huyu jamaa ana bahati sana, hivi wananchi wangeamua kujichukulia sheria mikononi kama ilivyo kawaida yao si angeshakuwa Marehemu? Alafu hana hata wasiwasi anaongea kwa kujiamini utafikiri alilofanya ni jambo jema.
Video kwa hisani ya Blog ya Kennedy.