Ikiwa leo ni siku ya upigaji kura nchini Tanzania..... Watanzania wote popote pale ulimwenguni tuungane kwa pamoja tuliombee Taifa letu ili uchaguzi uwe wa amani,utulivu na haki.GOD BLESS TANZANIA.
Ikiwa leo ni siku ya upigaji kura nchini Tanzania..... Watanzania wote popote pale ulimwenguni tuungane kwa pamoja tuliombee Taifa letu ili uchaguzi uwe wa amani,utulivu na haki.


Mmmmmh hapa nahisi wazazi ndio mashabiki na sio hao watoto.....Lakini waswahili wanasema mtoto umleavyo ndivyo akuavyo....
If you think massage is only for human being ,then you are totally wrong....Wanyama nao wanahitaji massage bwanaaa! kwani wao hawachoki?.... Ona huyo paka anayefanyiwa massage alivyotulia utafikiri ni Binadamu.......
Bango likiwa na ujumbe unaosomeka "SISI SOTE TUPIGANISHE UBAKAJI" Sina hakika kama neno TUPIGANISHE ni sahihi hapo, najaribu kujiuliza alikuwa anamaanisha awachukuwe wabakaji alafu awapiganishe au? Hapana bado haiingii akilini...Nafikiri angeweka neno TUPINGE labda lingeleta maana zaidi.


Watoto wa shule ya msingi wakiwa wamejitwisha mizigo ya kuni, wanakozipeleka mimi sijui....Sasa sijui ni adhabu au wanapeleka nyumbani na kama ni nyumbani wazazi wao wanafanya nini? Mimi nakumbuka nilivyokuwa darasa la tatu mpaka la tano nilikuwa nauza ubuyu wa mwalimu fulani hivi, na nikifanya kosa mwalimu huyohuyo alikuwa akinichapa na kunipa adhabu ya kumchotea maji ndoo tano nyumbani kwake. Nikikumbuka roho huwa inaniuma sana,huwa najiuliza kwanini nilikuwa nakubali kunyanyasika hivyo?
5O Cent now



